UGONJWA WA PID CHANZO DALILI , MADHARA NA SUKUHU YAKE

UFAHAMU UGONJWA WA PID KWA WANAWAKE DALILI MADHARA NA SULUHU.

BAADA yakupokea maswali mengi kutokana kwa kina mama kuhusiana na maradhi haya ya PID leo nimeamua kutolea ufafanuzi. Nimepokea simu nyingi na jumbe kupitia whatsap baada ya kuandika ile makala inayohusiana na madhara ya njia za uzazi wa kisasa.

PID ni maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke kama vile, mfuko wa uzazi, mirija ya mayai, vifuko vya mayai, shingo ya kizazi. 

               VISABABISHI VYAKE

Ugonjwa huu kwa kawaida husababishwa na maambukizi kwa njia ya kujamiiana, na mara nyingi hata magonjwa yanayohusiana na kujamiana huusishwa kama kama vile Pangusa ,UTI, Fangasi, Kisonono, nk. Pia utoaji mimba usiosalama, kuharibika mimba, au kujifungua kwa njia zisizo salama na kuweka vitu ndan ya uke kama vizuizi vya mimba pia huchangia maradhi haya.

DALILI ZAKE

Dalili za ugonjwa huu huwa kama ifuatavyo:


• Maumivu katika tumbo la chini na sehemu za nyonga.


• Kutokwa na uchafu mwingi wenye harufu mbaya sehemu za  uke.


• Kupata hedhi Mara mbili ndani ya mwezi.


• Kuhisi maumivu ama kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa.


• Kuhisi homa na baridi


• Kuhisi kichefuchefu


• Maumivu makali wakati wa kukojoa.


Ugonjwa huu unaposhindwa kutibiwa mapema unaweza kusababisha madhara makubwa kama ifuatavyo:


Kuota tishu katika mirija ya mayai, Mirija ya mayai kuziba, Vifuko vya mayai kukusanyika maji kwa ndani na Ugumba

Kuna njia kadhaa za kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi. Njia hizi ni pamoja na


Kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu au kama ikiwezekana kujizuia kabisa kufanya ngono.


Kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza au pindi tu unapogundua kuwa mwenzi wako ana dalili za magonjwa ya zinaa

Kufanya vipimo mara kwa mara hasa vya mfumo wa uzazi, pamoja na vipimo vya maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono (STI).

Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua, mimba kutoka au mara baada ya kutoa mimba ili kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga vema.

Tiba ya maradhi haya yanapatikana kwenye vituo vya afya hasa vinavyohusiana na masuala ya uzazi. Kuna dawa ambazo zimeidhinishwa na shirika la afya ulimwenguni unaweza ukapatiwa.

Au kama umeshatumia sana hukupata matokeo wala nafuu tunakukaribisha kwenye dawa za asili utapatiwa tiba kulingana na ukongwe wa tatizo

KWAHYO KAMA YUWAHITAJI DAWA TAFADHALI FANYA MAWASILIANO KWA NAMBA ZILIZOWEKWA PIGA ZUNGUMZA SHIDA YAKO UTAULIZWA MASWALI ILI KUJUA UKONGWE WA TATIZO 

TATZO CHINI YA MWAKA DAWA NI ELF 55000 MATUMIZI NI SIKU 21, MIAKA MWILI NA KUNDELEA NI ELF 80000 NA SIKU ZA MATUMIZI NI SIKU 42 JITAHIDI KUSOMA MAELEZO KWA UFASAHA

Tatizo hili husababisha matatizo ya uzazi, huendana na chango uvimbe kwenye kizazi ama mirija kuziba wakati mwingine hedhi kusumbua au kukata kabisa

+255621442936




Comments

  1. Mimi nasumbuliwa nahuu ugonjwa nataka kufahamu Tina yake

    ReplyDelete
  2. Nasikia maumivu upande was kushoto was nyonga baada ya kushiriki tendo la ndoa je ni dalili moja wapo ya pid?

    ReplyDelete
  3. Tafadhali nahitaji kujua ili nianze matibabu

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI