SIKU NA MILKI ZAKE, FAHAMU KUHUSU MALAIKA, JINI NA SAYARI ZINAZOBEBA SIKU

MAKALA HAYA YANAONGELEA MILKI ZA SIKU. YAANI JINI MALAIKA NA SAYARI ZINAZOMILIKI SIKU. NITAFAFANUA SAYARI NA NYOTA ZENYE UWEZO WA KUWA NA NGUVU KWA SIKU HUSIKA PIA NA MATUKIO MUHIMU UNAYOWEZA KUYAFANYA.

Katika tiba kuna siku na saa maalumu ambazo kuna kazi zikifanyika huwa na mjibu mujarabu. Yaan kuna kazi zikifanyika siku fulani muda fulan basi majibu yake huwa ni mazuri na hafaka zaidi kuliko zikifanyika siku zingine za kawaida.
ww.tabibuasili.blogspot.com

Hapa chini nitaongela siku na yanayohusiana na siku hiyo hivyo jitahidi kuwa makini sana katika kusoma. Kila siku zinakuwa na masaa ya kazi ila kuna siku maalumi kwa kazi maalum hivyo umakini wahitajika ukiwa wasoma. Nitafafanua kuhusu masaa buhuri dua na makafara.
                  SIKU YA JUMATATU

  Siku ya Jumatatu inatawaliwa na SAYARI ya QAMAR au KAMAR 'Moon'. Sayari hii ipo mbingu ya kwanza, Malaika wake  ni JIBRIL na jini wake ni MURRATUL ABYADH. Jini huyu na malaika wake hutawala siku ya leo mchana na Alhamisi Usiku.   Kwa pamoja  huibeba Nyota ya KAA kama ni nyota yake kuu. Hivyo watu wa nyota ya KAA siku ya Jumatatu ni siku ya bahati kwao.

         SHUGHULI MUHIMU ZA SIKU HII

Siku hii ni siku nyeupe hivyo ni nzuri kwa kufungua vifungo ama kuanza kazi za kitiba, pia ni siku nzuri kusuluhisha masuala ya kimapenzi kwa waliogombana. Pia kuna ndoa kwa watu wa Kaa pia ni siku ya vita.

Sayari ya KAMAR  inahusika na Kilimo, Kupata riziki, Safari, Mapenzi, Unyonge, Udhaifu, Ajizi, Khabari za uongo  Uenezi wa habari ambazo hazina msingi, Kufanya vitu kwa vishindo na haraka, Kufanya siri, Kuvunjika makao, Kuvunjika biashara, Kuingia kwa viongozi na Kutimiza haja.

 MASAA NA KAZI ZAKE SIKU YA JUMATATU

*KUSULUHISHA MAPENZI saa nzuri kwa suluhu za kesi za mapenzi bimaana wanaotaka kurejeana ama kuanzisha mahusiano, masaa mazuri ni saa moja asubuhi, saa tatu asubuhi, saa saba ni saa nzuri ya kumfunga mtu akili kimapenzi hasa masuala ya hirizi. Saa nane kwa wale wanaofunga ndoa ni njema hasa kwa watu wa kaa.

* KAZI ZA KUROGA  saanzuri kwa vita ndani ya siku ya jumatatu ni  saa mbili asubuhi hasa uhasma wa watu muunganiko iwe mapenzi ama mahirikiano ya kazi ya biahsra kugombanisha, saa nne asubuhi na saa tano hizi ni njema  kuanzisha vita ya uhasama ama kurejesha mapigo kwa aliyekuanza na kafara ya vita hyo apatikane mnyama mweupe kwa minajili ya sayar husika.

*KUSHUGHULIKIA MAJINI   saa nzuri kwa siku ya jumatu kwa wale wanaosumbuliwa na majini. Kuwapandisha ama kuwasikilza ama kuwfukuza muda mzuri ni saa sita mchana. Pia kama unataka kutuma kitu ama kufanya kazi kwa kutumia jini.

*KUOMBA UTAKACHO   saa nzuri kuomba kitu kwa mtu au kuzungumza na mabosi ama wakubwa kukidhiwa haja ni saa 12 jion. Hapa kuomba ama kutaka kitu kwa mtu 

*FUNGUO YA SIKU  saa 12 asubuhi ni saa ya kuomba shida zako muhimu kwa Muumba wako. Saa tisa pia huru kufanya kitu chochote kile kiwe kibaya ama kizuri utapata majibu haraka. Usiku wa Jumatatu ni nzuri kuomba heri ama toba kwa kile ulichokosea. Kuomba kupata kitu ambacho huna. Wenye imani  ni siku nzuri kwa kufunga sunna.

Uradi wa siku ya Jumatatu ni YA FATAHU YAA ALIMU isomwe mara 321 buhuri yake ni Ubani wowote changanya na Ubani Makka. Kafara lake ni mnyama mweupe asiye na doa


                       SIKU YA JUMANNE

SAYARI ya siku ya Jumanne ni MIRIKHI 'MARS' Sayari hii ipo Mbingu ya pili, Malaika wake ni IZRAEL, Jini wake ni ABUU MUHRIZ ambaye hutawala siku ya Jumanne kutwa nzima na siku ya IJUMAA Usiku. Huzibeba kwa kila kitu Nyota ya PUNDA na NG'E. Hivyo ni siku ya bahati kwa nyota hizo zilizotajwa.

SHUGHULI MUHIMU ZA SIKU YA JUMANNE

 Siku ya Jumanne inakiza na imekaa kiuadui sana hivyo inaaminika kila jambo utakalolifanya halina mwisho mwema ndani yake. Wapo wanaoamini usisasfiri wala kuanzisha jambo lolote siku hii. Ila ni muhimu sana kwa watu wa Punda na Ng'ombe kwani kuna siri kubwa katika mafanikio yao.

MASAA NA KAZI ZAKE SIKU YA JUMANNE

FARAQA, KUTENGANISHA jumanne imekaa kiuadui zaidi hivyo mida ya kugombanisha watu au kutenganisha muda mzuri ni saa moja asubuhi, saa nne asubuhi, saa nane mchana na saa 11. Masaa haya yamesimamia uadui hasa wa kuroga kutuma uchawi ama kutuma majini wabaya kwa kazi maalum.

KUSHUGHULIKIA KAZI kuna watu wanaugumu wa kukosa kazi na wamehangaika sana sasa ukishashughulikiwa mambo yako ya msingi yaan chanzo cha tatizo. Muda wa kutumia dawa kwa ajili ya kupata kazi kwa siku ya jumanne. Masaa yenye nguvu kwa siku ya jumanne ni saa sita mpaka saa saba mchana. Unaweza tumia kuoga dawa ama kwenda kwa watu waliokuahidi jambo baada ya kushughulikiwa. Saa 9 mura mzuri wa kukumbushia kazi au pesa.

UADUI KUTUMA  hii ni tofauti na masaa ya hapo juu masaa haya na ya uadui tu wakumsudia mtu mmoja sio kufarakanisha yaweza kuwa uadui wa kuroga, kuua, ama kudhuru ila kwa mtu mmoja. Muda mzuri ni saa mbili asubuhi.

MAMBO YA MAPENZI  kwa kesi za mapenzi muda kumdhibiti mtu ni saa tatu asubui. Saa tano ni muda mzuri wa kuoga dawa kwa wenye mikosi ya kimapenzi, saa kumi muda wa kuanzisha vita vya kumrejesha aliyekuacha. Saa kumi na mbili muda muafaka wa limbwata kutengeneza.

FUNGUO YA SIKU siku hii imekaa kiudui zaidi, hivyo saa 12 alfajiri ni saa nzuri kwa watu waliodhulumia ama kuibiwa. Mlilie Mungu wako kama kuna dawa ama mafanyo fanya wakati huo. Usiku wake ni mzuri kwa watu wenye mambo mazito ya kazi ama kutofanikiwa au kudhulumiwa.

Uradi wa jumanne ni YAA SAMIU isomwe mara 1121 dua Ganjul Arsh isomwe mara 7usomwe mara buhuri yeke ni Qist na kafara la siku hii ni Mnyama Mweusi.


                 SIKU YA JUMATANO

SIku ya Jumatatu inatawaliwa na Sayar ya UTWARIDI 'MERCURY' ambayo ipo mbingu ya pili . Malaika wake ni MIKYAIL na jini anayetawala siku ya leo ni BARKAAN. Kwa pamoja huzibeba Nyota ya Mapacha na Mashuke. Hivyo Jumatano ni siku ya bahati ya nyota ya Mapacha na Mashuke.

SHUGHULI MUHIMU ZA SIKU YA JUMATANO

Siku ya Jumatano ni siku nzuri ya kuwafukuza maadui au kuwapatanisha mke na mume, wapenzi au Marafiki waliogombana au kama wewe ni kiongozi wa Nchi ni siku nzuri kuanza kukusanya majeshi kwa ajili ya kulpa kisasi. Siku ya kuwapa uhuru wa kusona watoto. Siku ya kuenz vtu vya zamani usinunue kitu wala kuvaa nguo mpya yaweza kukuta majanga imekaa kimitego kwenye kupokea.

Sayari ya UTWARIDI inahusika na mambo yanayohusiana na Adabu, Malezi mema, Mantiki, Kupata kitu, Fasihi ya lugha, Ufahamu, Uelewa, Elimu, Urafiki, Hila na kudanganya, Hesabu, Vitabu, Sanaa za aina zote, Ukatibu au Ukarani, Shule au Kumpeleka mtoto shule. Pia mambo ya Nakshi, masuala ya Urembo na kuandaa majeshi

MASAA NA KAZI ZAKE SIKU YA JUMATANO

MASUALA YA MAPENZI  saa ya kushughulikia mapenz bimaana kupatanisha au kuunganisha ni saa moja asubuhi, saa mbili asubuhi na saa kumi jioni. Kwa wanaume saa saba ina nguvu sana kushughulikia masuala ya wanawake. 

KAZI ZA KINGA  jumatao unaweza kukinga nyumba shamba mwili ama mali yoyote zingatia visomo kama unafuata visomo na makafara saa inayokupa nguvu na majibu haraka ni saa nne asubuhi.

KAZI ZA KUROGA  kufarakanisha watu makundi ama ndoa siku ya jumatano ni saa tano  asubuhi. Ikiwa kufarakanisha mtu unayemmiliki ana mchepuko ni saa sita mchana.

KUMUOPOA MGONJWA ikiwa umepata mgonjwa wa kumtibia na tiba yake yahitaji kunywa anza mishale ya saa tisa kuandaa dawa na kukusanya vifaa kwa ajili majibu ya kile kilichosudiwa. Saa kumi na moja ni saa ya kunywa dawa pia saa ya kurudisha mapigo

FUNGUO WA SIKU  katika siku ya jumataton kuna masaa yapo huru kufanya jambo lolote liwe la heri ama shari kikubwa ni kufuata sheria za jambo unalotaka kulifanya. Saa tatu asubuhi inakupa jibu unalotaka. Saa 12 ni muda wa kwenda kuzungumza na watu wenye wadhfa kwa ajili ya msaada maalumu. Jumatato usiku ni siku nzuri kwa matambiko watu wenye shida za asili kuhusiana na matambiko wanaweza kuzungumza na mizimu yao kwnye ndoto. Usifanye jambo lolote saa nane mchana ni saa ya mushker hakuna kinachomea.

Uradi wa siku ya Jumatano ni  YAA GHANIYU YA ADHWIMU isome mara 1111, buhuri yake ni kafara lake ni Mnyama Mwekundu.


                      SIKU YA ALHAMISI

SAYARI inayoongoza siku ya Alhamisi ni  MUSHTARA. Sayar hii ipo Mbingu ya sita Malaika wake anaitwa ISRAFEEL  jini wake anaitwa SHAMHURUUSHS ni Kadhi wa Majini na anatawala Alhamisi mchana na Jumapili Usiku. Nyota zenye nguvu na bahati leo ni MSHALE na SAMAKI

SHUGHULI MUHIMU ZA SIKU YA ALHAMISI

Siku ya leo Alkhamisi ni siku nzuri ya kufanya
kazi ya udobi, kununua na kuuza, kutoa mali na kuingiza mali ni siku nzuri ya kuanza kazi,
kupunguza nywele na kuingia kwa wakubwa na
wanawake. Siku njema kuhamia nyumba mpya siku ya kuhukumu watoto wako waliokukosea.

Pia ni siku nzuri kwa safari za baharini na bara na kuanza kuandika kitabu na kufungua ofisi na kusoma vitabu na kufundisha.

Sayari hii ya MUSHTARA inahusika na
Ulaini, Urahimu, Akili, Elimu, Upole, Mambo ya Serikali, Ukarimu,  Unadhifu wa mwili na nguo na Kuingia kwa wasomi na Kutembelea Wizara.  Pia husimamia uongo ama utapeli hivyo umakini unahitajika kwenye safari za knunua na Kuuza, kuoa, Kupata elimu kugombea ugomvi. Huambatana na ugonjwa wa shinikizo la damu.
   
     MASAA NA KAZI ZA SIKU YA ALHAMISI

KUANDIKA TARASIMU ikiwa kwenye matibabu yako kunahitajika tarasimu ama kombe basi siku nzuri ya kuandika ni alhamisi, na wasaa mzuri ni mchomozo wa jua kuanzia saa moja asubuhi. Haya yanahusiana na mahaba ama kutoa sihiri au kwa ajili ya kuharakisha kazi ama kutoa nuski.

KAZI ZA MAPENZI  muda mzuri kwa kesi za mapenzi kwa siku ya alhamisi ni  saa sita mchana,saa nane mchana,  saa kumina moja na saa 12. Masaa yote hapa ni mazuri kwa kesi za mapezi iwe kurejesha kuvuta kumaliza kasi kumdhibiti mtu pia milango ya ndoakwa siku ya alhamisi husimamia masaa hayo.

MLANGO WA MBAYA pia siku hii kuna saa nzuri na mbaya kwa mapenzi iwe kindoa ama kushughulikia dawa za mapenzi. Saa tano asubuhi na saa kumi jioni sio wakati mzuri ni mlango wakutoka hivyokama inataka kumpiga mtu uadui wa kimapenz ama kuvunja mapenz baina ya watu saa hiyo ninzuri zaidi. Hata saa mbili asubuhi pia huingia kwenye mlango wa kutokea ni saa ya kupataau kukosa ukicheza kamari muda huo utaliwa.

MLANGO WA KHERI kuna wakati pia ukifanya jambo lolote linajibu mfano saa tatu asubuhi mlango wa kutoka, unaweza kuanzisha safar kufanya dua ama kuanza biashara. Saa nne asubuhi ni muda wa mabosi kama kwenda kuomba jambo ama kuwaroga ili uwadhibiti. Muda wa kukoga dawa za kupanda cheo ama kupata kazi unayoiomba kwa muda mrefu

KUSHUGHULIKIA MAJINI  muda mzuri wa kushughulikia majini kwa siku ya alhamisi ikiwa ni kuwapandisha, kuwafukuza nk ni saa saba mchana. Andaa vtu vyako muda ni huo kushughulika na mambo wa majini.

UADUI WA KAMAPENZI saa tisa ni nzuri kwa kutenganisha ama kushughulikia uadui wa kimapenzi

FUNGUO YA SIKU siku ya Alhamisi usiku ni nzuri kwa kupata taarifa za kijini. Usiku kabla ya kulala unaweza kufanya dua ama kuwaomba majini wakupe taarifa. Hata wanaosumbuliwa na majini ya ukoo mizimu siku hii usiku ni njema kushughulikia mambo haya.

Uradi wa Alhamisi ni YA KABIR YA MUTAA'L isomwe mara 773  buhuri yake ni UDI KAFUUR kafara lake mnyama aliyechanganya rangi zisikosekane nyeupe na nyekundu.

  
                        SIKU YA IJUMAA

SAYARI ya siku ya Ijumaa ni ZUHURA, Sayari hii ina jinsia ya kike ipo mbingu ya mm Malaikwa wake anaitwa ANN-YAIL-ANAEL. Jini wake ni Al ABYADH. Nyota zenye nguvu na bahati siku ya Ijumaa ni Ng'ombe na Mizani.

 SHUGHULI MUHIMU ZA SIKU YA IJUMAA

Siku ya Ijumaa ni siku nzuri ya kuoa, kuanza urafiki na mwanamke, kufanya tendo la ndoa, kusafiri, kufanya biashara, kupenda, mambo yote ya raha utakayofanya katika Siku hii ni mazuri na yenye baraka.

Sayari hii ya Zuhura inahusika na Muafaka, Urafiki, Uzuri wa moyo, Mapenzi, Masikilizano, Mapatano, Tabia nzuri, Mambo ya muziki, Starehe, Michezo na kila kitu chenye kufurahisha mwanamke.

MASAA NA KAZI ZAKE SIKU YA IJUMAA

MASUALA YA MAPENZI Siku hii ina nguvu sana kwa wanawake kuwashughulikia wanaume kimapenzi. Muda mzuri wa kufanya kazi zinazohusu mapenzi ni saa moja asubuhi kazi yoyote utapata jibu. Saa tatu ni saa kujishughulikia mtu aliyeachwa hivyo kama kukoga dawa ama kujifusha ni nzuri. Saa sita ni nzuri kwa kufunga ndoa ama kuanza shughuli za posa. Saa nane ni njema kwa ndoa ama kushughulikia masuala ya kimapenzi pia. Saa nyingine ni saa kumi pia ina nguvu katika mapenzi ya kindoa na shughuli za dawa. Saa kumi na mbili ni mdua mzuro wa dawa za kutoka kama umepewa dawa yatajiwa ifanyike nje au utoke nje ya nyumba yako bimaana porini ama sehm yoyote saa 12 ni nzuri hata kwa ndoa pia mujarrab hasa kwa mwanaume inakupa nguvu ya kusikilizwa isipotuke saa moja.

FARAQA NA VITA  kama una vita basi saa mbiki ni muda muafaka wa kuangalia hiyo vita ukubwa wake pia waweza kuanza mashambulizi hasa vita vyenye asili ya uchawi. Kama imebidi kutengenisha watu bsi saa nne ni mujarrabu huwa haipinduki.

KUKIDHI HAJA Siku hii ina mambo mengi sana hivyo kama yuwataka kuomba kitu kwa mtu ama yuwamdai ama unataka kazi basi mida mizuri ya kufanya dua ama dawa kwa ajili ya mambo hayo ni saa tano asubuhi, saa saba mchana. Mida hiyo unaweza pia kwenda kuomba ama kuwalilia watu shida ni mida ya kupewa unachotaka.

MILANGO YA KUTOKA Kama una safar siku ya Ijumaa nsi muda mzuri ni saa tisa ikiwa ni safari ya kwenda mbali. Saa 12 asubuhi huto mwangaza mzuri hivyo kama utaikosa saa 12 basa saa tisa ni njema. Hivyo kama umeoa ijumaa basi jitahd kutoka sehem ya ulipolea saa tisa ila hakikisha usioe muda wa saa tisa umeingia mlango wa kutokea hasa kwa watu wa nyota ya Mbuzi.

FUNGUO YA SIKU  Ndani ya siku hii imetawaliwa sana na mapenzi hivyo kama una shida yako muhimu fuatilia masaa yaliyowekwa ndani ya siku hii saa 11 jion ni saa ya funguo unaweza kuomba kitu chako kizito ukapata majibu. Usiku wa Ijumaa ni nzuri kwa watu kuomba radhi kwa yale mabaya waliyotendea wenzao. Pia ni siku ya kuzunvumza na majini ama kupata taarifa ya mambo yanayowasibu.

Uradi wa Ijumaa ni YAA MALIKI, YAA QABEER dua yoyoye kulingana na shida uliyonayo inakupa majibu buhuri yake ni uban Mashataka. Kafara lake ni Mnyama asiye chini ya miaka miwil asiwe mlemavu mwenyw rangi zaidi ya mbili.

                     SIKU YA JUMAMOSI

SAYARI inayobeba siku ya Jumamosi ni ZOHALI, Sayari hii ipo mbigu ya jini wake anaitwa ABUU NUHU, Malaika wake ni KAYFIL  hawa hutawala zaid Mchana wa siku ya Jumamosi na usiku wa siku. Nyota zenye nguvu na bahati siku ya Jumamosi ni Ndoo na Mbuzi.

SHUGHULI MUHIMU ZA SIKU YA JUMAMOSI

Siku hii imekaa kivisasi uadui wa kuadhibu, kulipa ubaya, kuanzisha vita ama mipango ya kumdhoofisha adui. Kugombanisha watu katika mapenzi kufafakanisha. Sio siku nzuri kuanzisha mambo ya heri isipokuwa kwa watu wa nyota ya Mbuzi na Ndoo.

MASAA NA KAZI ZAKE SIKU YA JUMAMOS

MAMBO YA MAPENZI  muda mzuri wa kufanya dawa za mapenzi ya kuvuta kwa siku ya jumamosi ni saa mbili asubuhi, saa nne na saa sita mchana na saa 12 jion. Wakati muda mzuri wa kufunga ndoa kwa watu wa Mbuzi na Ndoo ni saa tano asubuhi.

UADUI WA MAPENZI  muda wa kutengenisha ama kufarakanisha watu ni saa moja asubuhi, saa tatu asubuhina saa kumi jioni. 

KUKIDHI HAJA muda wa kwenda kwa wakubwa kuomba haja zako ni saa saba mchana. Hata saa tisa mchana ni nzuri pia husimamia watoto kama una watoto wataka kuanzisha kitu wasaa huo ni mzuri.

SAAA YA ELIMU kama una jifunza jambo ama yuwataka kuanzisha safar za kielimu basi saa tisa ni njema kwako.

MAMBO YA KIJINI NA UCHAWI  saa nane mchana ni muda mzuri wa kushughulika na kesi za majini ikiwa ubaya unautaka kuufanya kwa kumtuma jini basi wakati huo ni mzuri. Saa 11 inasimamia uchawi wa kijini hapa kutoa na kuwatuma ama kubatwikishwa.

FUNGUO YA SIKU saa nne asubuh ni muda uliokuwa waz ukifanya jambo lolote liwe la heri ama shari majibu utayapata mujarab muhimi ni kufuata mashart ya siku husika. Usiku wa Jumamosi ni usiku wa vita hivyo kama yuwataka kumuita jini kwa ajili ya mambo ya kivita uadui kwa watu basi ni njema muhimu uwe na maelekezo ya kitaalam au usimamizi.

Uradi wa siku ni YAA HAKEEM isomwe mara 721 buhuri yake ni mafusho machafu yachanganywe na Miatun Saila kafara lake mnyama mwenye rangi nyeusi ama mwenye baka jeusi usoni ama tumboni


                      SIKU YA JUMAPILI

Sayari inayobeba siku ya Jumapili ni SHAMSI, Sayari hii ipo Mbingu ya nne ina jinsia ya kiume na asili ya moto. Malaika wake ni RAUKAYAIL na jini wake ni ABDULLAH SAEED MADHAAB. Jini huyu anatawala mchana wa siku ya Jumapili na Usiku wa siku ya Jumatano.  Nyota yenye nguvu na bahati siku ya Jumapili ni Simba. 

  SHUGHULI MUHIMU ZA SIKU YA JUMAPILI

Siku nzuri kwa kuomba msamaha kuanziaha mahusiano ndoa. Mwanaume ndiye siku yenye nguvu zaidi kwa mambo yako ya siri,mwanamke ni siku yenye nguvu zaidi kwa kumdhibiti mwanaume. Ni siku ya malipo siku ya fuaraha ni miomgoni mwa masiku meupe.

   MASAA NA KAZI ZA SIKU YA JUMAPILI

MASUALA YA MAPENZI Siku hii ina nguvu sana kwa kumroga mwanaume. Yaan mwanamke mwenye shida za kimapenz basi siku ya Jumapili ni nzuri kwake. Saa ya kushughulikia kesi za kumuweka karibu ama kumvuta mtu ni saa mbili asubuhi na saa 11 hapo kwa wale ambao wanataka watu wawe wao ila hawapo kwenye mahusiano nao. Kumrejesha mtu aliyekuacha muda mzuri ni saa tatu asubuhi na saa nne asubuhi. Wakati muda wa kufanya dawa wewe upendwe kwa siku hii ni saa nne asubuhi pia inaingia, saa tisa mchana na saa 12 jioni. Muda wa kumfanyia ubaya mtu aliyekutesa kimapenzi ni saa moja asubuhi.

FARAQA KUROGA  Siku ya jumapili pia kuna muda kazi za kuroga ama kugombanisha huitika. Mfano saa moja asubui ukitaka kulipiza ubaya kwa mtu aliyekuroga unaenda. Saa tano asubuhi unaweza kufarakanisha watu aidha mapenzi ama kundi la watu lenye maslahi. Pia saa tano unaweza kumpa mtu nuksi ahangaike nayo. 

VITA NA KINGA Kwa walio kusudiwa ubaya wa kutupiwa ama kurogwa unaweza kuitumia saa saba kurejwsha vita yaan kurwjwsha manibu kwa yale uliyofanyiwa pia ukaitumia saa nane kwa kutafuta kinga ya mwili hasa kupandiahwa miliami ama kwenye miti mikubwa.

FUNGUO YA SIKU  Jumapili ni siku nzuri kwa kufanya biashara maalumu kama kuuza mali yako ama kununua na muda mzuri hasa ni saa 6 mchana. Muda wa kufanya jambo lolote la heri ni saa nne asubuhi. Pia kwa wenye mazito makubwa hayaishi kama una dawa maalum umeandaliwa basi oga saa tisa mchana pia kuna heri. Usiku wa Jumapili ni mzuri kwa kazi za kurejesha vitu vilivyopotea ama dua za kukomesha wezi.

Uradi wa siku ya Jumapili ni YAHAYU YA QAYUMU isomwe mara 173. Buhuri yake ni SANDARUSI kafara lake ni mnyama Mwekundu au kahawiya.

MAKALA HAYA YAMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA MTABIBU ASILI TZ. NI UFAFANUZI NA MAELEZO KWA SHIDA UNAYOTAKA KUIFANYA UNAANGALIA SIKU GANI INA NGUVU ZAIDI. MASAA NI YAPI URADI WAKE BIMAANA DUA ZAKE NA MAKAFARA YANAYOHUSIKA. HAYA WALE WATU WAKUCOPY NA KUPASTE ELIMU NI HIYO KAZI KWENU.

MFANO UNATAKA KUNSHURUTISHA MTU KIMAPENZI NI LAZIMA UJUE ASILI YA NYOTA YAKE UJUE SIKU KWAKE UAUDUI USIMAMA. NA NDANI YA HIYO SIKU MUDA GANI HAPO UKIFANYA KAZI YAKO UNAKUWA NA MAJIBU AMA MATOKEO YENYE UHAKIKA KILICHO BAKI NI QADAR ZA MWENYEZI MUNGU. HIVYO KUWA MAKINI KATIKA KUANDAA KAZI ZAKO KWA WATEJA KUWA MAKINI WAKATI UNATENGENEZEWA JAMBO LAKO.

PIA KUNA ELIMU YA TARASIMU YA KHATAM SULEIMAN AMBAYO INATOA MWANZO WA TARASIMU KWA ZILE ALAMA ZA KINYOTA NA SIKU HUSIKA KWA MARADHI MIKASA YA MAPENZI NA MASUALA YA NYOTA KWA WAHITAJI FANYA MAWASILIANO KWA NAMBA ZANGU

KWA WAGONJWA ANGALIA VIZUR UGONJWA WAKO SIKU GANI UNA NGUVU YA KUTIBIWA.

UNA SHIDA YOYOTE YA NYOTA, BIAHARA, KAZI, MAPENZI, KESI, KUIBIWA, UZAZI, NGUVU ZA KIUME, KUKUZA DHAKAR NK PIGA SIMU KWA NAMBA

+255621442936

KAMA UNATUMA UJUMBE BASI WEKA MAELEZO YA KUTOSHA JINA PAHALA UNAPOISHI NA SHIDA HUSIKA. JUMBE FUP KAMA MAMBO NIAJE HELLOW VIPI SITAZIJIBU

Facebook page



Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI