NDOTO ZINASHOARIA UCHAWI, KUROGWA NA KUCHUKULIWA MSUKURE

NDOTO ZINAZOASHIRIA UCHAWI, KUROGWA, MSUKULE

 KUna ndoto ukiota inaashiria wewe muotaji umerogwa au unataka kuingizwa kwenye chama cha wanga au unataka kutolewa msukule kuwa makini katika usomaji. Kuna hatua kama nne kuu za mtu kuingizwa kwwnye wanga hizi nitazizungumza siku nyengine mungu akitupa uhai leo tuangalie hizi ndoto na tafsiri yake.


Ukiota nyoka mweusi amekuingia mwilini kwa aina yoyote ile iwe kapitia miguun kichwani mkononi tumboni ni ishara ya kuingiwa na jini wa kichawi ambao ametumwa na wachawi.

Ukiota unakula nyama na ndoto zikawa zajirudia mara kwa mara ni ishara ya kulishwa vitu vibaya na wachawi usiku sasa aidha wanakulisha kwa kukudhuru au wanataka kukuingiza chamani. Hapa hata ukiamka asubuhi msomo huhisi kweli ulikula kitu usiku.

Kuota unaingiliwa kimwili mara nyingi waenda usiku anaweza akakutongoza mchana ukakamtalia basi huja kukuadhibu usiku utaota unaingiliwa na mtu tena kwa fujo na ukiamka hujikuta umechoka  na umechafuka na wakati mwingine hukuingilia hata kinyume na maumbile hii hata wanaume hufanyiwa.
Hapa tufahamiane kidogo wanaume nao huota wanamuingilia mwanamke wakati mwingine mtu mzima au pia huota wao wanaingiliwa kinyume na maumbile na wanaume wenzao.
Pia wanga hutumia shahawa za mwanaume kama dawa za kuwadhuru watu huchanganya na vtu vingine. Wanakuja usiku  wanakufanyisha mapenzi ukitaka kukojoa wanakinga shahawa wanaondoka nazo.

Ukiota upo kwenye sherehe kubwa sana 
Katika hatua za kuingizwa kwenye chama hii na hatua za mwisho mwisho utaota watu wapo kwenye ngoma na wewe upo unawaona watu usiowajua na unaowajua kuna vyakula vyapikwa wewe utafanywa kama mgeni rasmi pale utatambulihwa watu wengine ndugu yangu ikifikia hatua hii wahi mapema kwa wataalam wewe mpaka chale ushachorwa.

Ukiota ngoma ukiota upo kwenye ngoma za asili ndogo tu ila kuna vtu vya asili vya kimila na watu wanakusherehekea sana ni dalili pia ya kuinhizwa chamani japo hii huyofautina na mazingira wakati mwingine huashiri matambiko ya ukoo.

Una mgonjwa au wewe mwenyewe unaumwa ukaota mtu kashika chungu chenye damu alaf ameshika kitu kitamu ambacho wewe au mgonjwa hupenda kukila ni ishara ya kuchukuliwa msukule pia ukiota unaitwa usiitike ukiota miruzi mingi usiku ukiota upo kwenye miti ukiota juu ya ungo ni ishara mbaya

Ukiota upo kwenye gari unasafiri alafu watu wapo uchi kwenye hilo gari pia ni ishara ya kuingizwa uchawini


Waliolishwa uchawi mara nyingi miili huuma vichomi kuhisi vtu kutembea mwilini mwili kufa ganzi mwili kupoteza nguvu kuishiwa damu nk dawa za kutoa uchawi zategemea na aina ya uchawi ulofanyiwa fika kwa wataalam karibu nawe au nitumie ujumbe inbox ukihtaji msaada wangu

Vitu vyakuzingatia jikinge mwili wako, kinga nyumba au chumba chako au eneo lako la klbiashara fanya sana visomo sali sana mungu atakuwa pamoja nawe.


Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI