ASILI ZA MAJINI FAHAMU KUHUSU JINI CHEKETU


MUENDELEZO wa mfululizo ya asili ya majini katika kuwafahamu namna wanavyofanya kazi na jinsi wanavyoathiri watu. Leo tutaongelea kuhusiana na jini huyu Cheketu. Jitahd kusoma kwa umakini mwanzo mpaka mwisho anayekuletea darasa hizi ni Mtabibu ASILI TZ.

Kwa ujumla majini wanakuwa na asili zao kama unavyoona asili za makabia yaliyopo kwenye nchi uliyopo. Wapo Majini Miliki ya bahari wapo majini miliki ya Bara kama tuliyozungumza jana Mmasai. Wapo majini Wakristo Wapo majini Waslam wapo kitoka mabara mengine kama Uarabuni Ulaya nk we endelea kufuatilia darasa zangu utatanua uelewa wako na kutoongopewa kuhusiana na majini kamwe.


       SIFA NA ASILI YA JINI CHEKETU 

HUyu ameondoka kwenye sifa za kijini amekuwa shetani. Miongoni kwa makoo maarufu Kishetani katika Ulimwengu wa Kijini. Shetani huyu ana sifa kubwa ya kiwa msanii yaan muigizaji ana uwezo wa kuogiza kila anachokiona kila anachokisikia na akakifanya kwa usawa uleule.

Shetani huyu asili yake ni Uchawi hivyo katika ulimwengu wa tiba hutumiwa na wachawi katika kufanikisha mambo yao ba hufanikiwa kwa asilimia kubwa. Kazi yake ni uovu na hujigeuza na kujifanya jini mzur anapomuingia mtu ili isiwe rahisi kugundulika. Ana uwezo wa kujifanya Mmasai Sharif Ummu Subian na wengine kwa elimu ndogo unaweza usimfahamu kwakuwa ana uwezo wa kuigiza vyema.

Ana ufalme katika mashetani waovu na ana nguvu ya ushawishi kwa jeshi la kishetani hivyo anapopewa kazi na maagano yakawa mazuri kuna uhakika wa kutimia njama zake.

    NAMNA YA KUMPATA JINI HUYU

Katika majini wepesi kuwapata huyu ni miongoni mwao makazi yake ni majaani, makaburini, vyooni na  sehem wanazochezea watoto sana. Wachawi wana ishara zao za kumuita na kuingia nao maagano. Mchawi yoyote haweza kuingia kwwnye nyumba ya mtu kabla ya shetani huyu kumfungulia njia za kupita baada ya kupima uzito wa nyumba.

Uoatikanaji wake na Mchawi mkuu au mganga anayetumia uchawi anakupatia kwa akazi unayoitaka kumfanyia. Pia zipo njia za kurithishwa, iwapi mzee wako alikiwa mchawi basi anauwezo wakukurithisha ukoo wa shetani huyu nawe ukamtumia kwenye mambo yako. Ila sio jini mzuro na sishauri mtu kufunga safar kwenda kumtafuta sababu anatabia ya kubadilika anapoahidiwa kikubwa zaidi huko atakapokamatwa.

     CHEKETU KATIKA KAZI NA UMILIKI WA MALI 

jini huyu hatoi mali kazi yake ni kuharibu tu maisha ya wanadamu. Hajishughulishi sana na kuneemesha watu bali kuharibu mambo ya watu ikiwa utaelewana nae aweza kupatia nguvu za kuhribu na si kutengeneza. Watu wengi wanaomiliki jini huyu hawana maendeleo ya kuonekana sababu wapo kimaharibifu zaidi.

Mtu aliyekumbwa na jini huyu amakutupiwa kupona inakuwa ngumu mpaka umpate mtaalam mwenye ujuzi wa majini na si mtaalam mwenye kupanda majini. Sababu jini huyu anaweza kumhingia mgonjwa kisha akataka kujifanya anataka mgonjwa aague. Ila hatoi msaada katika kutafuta vitu anavyotaja utakatuta jini anataka pete ila wauguzi ndio mtafute pesa mnunulie atataka mshuka wauguzi ndio muharamie akipagiwa kila kiti bado mgonjwa anaendelea kuteseka.

Watu wengi wakimtoa baada ya muda anarejea tena sababu anakiwa amemtanguliza kibaraka wake nyinyi mwaona mmetoa jini kumbe mmetoa kibataka yeye anakaa pemben dawa zikisha nguvu anareja. Yatakiwa kazi ya ziada na muda wa kutosha kuandaa hivyo kwa wagonjwa mjitahd kutafuta suluhu.

Dalili zake ni Kuamka asubuhi na kukuta umechanjwa kwenye mwili wako, Mbavu Kuumwa Sana bila sababu yoyote, mwili kuchoka Sana bila sababu zozote, Kila unapoamka mwili unauma Sana au kiungo Cha mwili Kuwa uchungu Sana, Kila unapokaa au kutembea unahisi unafuatwa na kivuli Cha mtu, Kushituka shituka usingizini nyakati za usiku, Kupiga kelele usingizini. Kupandisha mashetani yasiyoeleweka leo anaweza akajifanya mmasai kesho akajifanya sharif. Wakat mwingine haongei analia tu chichichiii achukuchuku chuu ujue ni huyo ni mahepe.

Kuandamwa na ndoto za kula nyama, kukaa kwwnye vikao vya shughuli za asili. Kuota unaoanda ngombe kuota unaingiliwa kimwili au kuingilia. Kupaa ndotoni na mwenyewe ukaona raha sana. Humfanya mwanadamu kuishi maisha maguku kuwa na ahadi zisizotimia. Mahusiano kuvunjika. Kufilisika wakati mwengine huharibu uzazi nk.

Kazi zake kubwa na kuua kuchukua misukule wizi hatumiki kwwnye tiba ila udanganyifu wa kitiba.

     MADHAIFU YA JINI CHEKETU

KAMA NILIVYOELEZA HAPO JUU HUYU NI MSANII HIVYO ANAPOKUTANA NA WAJUZI ZAIDI HUKAMATWA KIWEPES. HIVYO ANAWEZA KUTOA SIRI ZA ALIYEMTUMA NA AHADI ALIYOPEWA, IKITOKEA AKAPEWA AHADI NZURI ZAIDI HUKO ANA UWEZO WA KURUDI KWA ULIYEMTUMA NA KUKUDHURU KILE KILE ULICHOTAKA AKAMDHURU MTU.

YASHAURIWA KUJIKINGA VYAKUTISHA KABLA YA KUFANYA KAZI NA SHETANI HUYU SABABU HANA MSIMAMO KATIKA KAZI ZAKE. HATOI MALI MAANA VIJANA WENGI KILA UKIWEKA HABAR ZA JINI WAO WANASHUPALIA MALI TU HUYU KAZI YAKE NI KUHARIBU WATU WENGINE.

CHANO AMA CHAKULA CHAKE NI VITU VICHAFU MABAKI YA VYAKULA VYA WATOTO. DAMU ZA HEDHI DAMU ZA KUHARIBIKA MIMBA NA HUPENDA KULAMBA MIKONO YA WATU PALE WANAPOTEMBEA.

DAWA YA JINI HUYU NI KUMTOA HIVYO ZINAHITAJIKA DAWA ZENYE NGUVU KULINGANA UKONGWE WAKE. ASISIKIKIZWE KUTIMIZIWA KILE ALICHOAHIDIWA ALIPOTUMWA MKIMPATIA MNAMFUGA ZAIDI. KWA UCHACHE DAWA MOAKA SIKU 21 HADI MWEZ MZIMA NDIPO HUTOKA.

UTARATIBU ULE ULE UNA SWALU KUHUSU JINI WEKA HAPO CHINI UTAPATIWA UFAFANUZI. SHIDA BINAFSI FANYA MAWASILIANO KWA NAMBA ZANGU.

Una shida yoyote ya kinyota, majini, mapenzi, biahsra, uzazi, nguvu za kiume, uzazi, oete za bahati nk

+255621442936

Kwa wale mnaoutuma ujumbe weka maelezo yakutosha, jina pahala ulpo na shida yako jumbe fupi fupi sitazijib

Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI