FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA SUKARI NA TIBA YAKE
FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA SUKARI NA TIBA YAKE
BY MTABIBU ASILI
UHALI gani mpenzi wa msomaji wa makala zangu ambazo zinalengo la kuimarisha afya ya binaadamu pamoja na urembo. Nimezungumza sana juu ya kupunguza Unene kwenye makala zilizopita lakini pia nlizungumzia kuhusiana na masuala ya afya uke ikiwa kuwa na maji, mkavu, hauna joto sambamba na vtu vingine.
Kama ulipitwa na masomo yaliyopita unaweza kutembelea ukurasa wangu au kuingia kwenye group la Afya ya Uzazi kwa njia asili.
Baada ya utangulizi huo mfupi sasa tuingie kwenye somo letu la leo linalohusiana na suala zima la ugonjwa wa sukari na tiba yake.
Sukari imekuwa ikiwatesa watu wengi hasa wenye umri zaidi ya miaka aeobaini japo kwa sasa imekuwa tofauti hats watoto wadogo wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huu.
Kwa kawaida binaadamu anatakiwa kuwa na sukari normal ikizidi inakuwa sukari ya kupanda ikipungua inakuwa sukari ya kushuka.
Leo nakupa njia za kutibu sukari kwa ujumla iwe ya kupanda au kushuka. Kwa kufuata taratibu hapo chini unaweza kumaliza ugonjwa huu.
Zifuatazo ni baadhi ya Tiba za ugonjwa wa sukari. Ukitumia kwa makini na kufuata masharti unaweza ukapona kabisa kwa kutumia njia hizi za asili.
1. J ELI YA MSHUBIRI
Unaweza ukatibu ugonjwa huu kwa kutumia jeli ya mshubiri. Kuandaa na kutumia dawa hii fuata maelezo hapo chini.
FAHAMU NJIA ZA KUANDAA SHUBIRI KUWA TIBA YA SUKARI
Changanya vifuatavyo kwa vipimo vilitajwa hapo chini
• Jeli ya mshubiri kijiko cha chai 1 • Unga wa majani ya matunda ya damu ya mzee kijiko cha chai 1 • Unga wa manjano kijiko cha chai 1
Kunywa mchanganyiko huu kila siku kabla ya chakula cha mchana na jioni maana yake ni Mara mbili kwa siku.
Dumu hivyo kwa majuma kadhaa mungu atakufanyia wepesi.
2. MAJANI YA MUEMBE
MWENYE ugonjwa wa sukari aruhusiwi kula embe mbivu kwa wingi kutokana na kiwango cha sukari kilichopo kwenye tunda hili. Lakini ugonjwa huu unaweza ukatibika kwa kutumia majani ya mwembe. Ili kutumia kama dawa fuatilia maelezo hayo hapo chini.
Loweka majani 10 mpaka 15 ndani ya nusu lita ya maji kwa usiku mmoja. Chuja maji haya asubuhi mapema na uyanywe kabla ya kula chochote. Subiri lisaa limoja lipite ndipo ule chakula cha asubuhi. • Kausha majani ya muembe kwenye kivuli. Yatakapokuwa yamekauka kabisa, yasage kupata unga wake na hifadhi unga huu katika chombo kisafi na kisha lamba unga huu nusu kijiko kidogo cha chai kila siku kabla ya chakula cha mchana na jioni.
3. UNGA WA UWATU
TAfiti nyingi zimeonyesha kuwa uwatu una uwezo mkubwa katika kutibu kisukari. Uwatu huzisisimua seli katika kongosho kitendo kinachofanya uzalishwaji wa insulini kuongezeka. Maajabu haya ya uwatu yanasemekana kufanyika kutokana na uwatu kuwa na asidi amino mhimu sana ijulikanayo kama ‘4-hydroxyisoleucine’. Miaka mingi kabla hata ya huu utafiti kufanyika, uwatu umekuwa ukitumika kama moja ya dawa bora kabisa za asili katika kutibu kisukari.
JINSI YA KUTUMIA UWATU KUTIBU SUKARI
• Chota mbegu za uwatu vijiko 4 na uziloweke katika maji robo lita kwa usiku mmoja. Asubuhi ponda ponda hizo mbegu za uwatu ndani ya maji kisha zichuje na upate maji yake. Kunywa maji haya kila siku asubuhi kwa muda wa miezi 2. • Chukuwa uwatu ya unga vijiko vikubwa 2 na uweke ndani ya maziwa au maji ya uvugu uvugu robo lita, koroga vizuri na unywe kila siku kutwa mara 2 kwa miezi 2. • Chukuwa gramu 100 za mbegu za uwatu na gramu 50 za binzari manjano. Unaweza kuongeza kiasi kidogo cha pilipili manga nyeupe kwenye mchanganyiko huu.
Ongeza kijiko 1 cha mchanganyiko huu wote katika maziwa robo lita na unywe kutwa mara 2 kila siku. • pia unaweza kutumia unga wa uwatu ukauchanganya na ngano na ukatumia kupikia bites na ukala
Kupata dawa zilizoandaluwa kwa ajili ya sukari 0621442936
Comments
Post a Comment