TIBA MAALUMU YA MAFUA NA MAPAFU KWA AJILI YA WATOTO
NAAM leo nitazuzngumzia kuhusiana na watoto. Juma lililopita nilizungumzia kuhusiana na mtoto anayelia usiku. Mashallah wengi waliofanya wamenitumia ujumbe kuwa watoto sasa wanalala vizuri.
Mara nyingi kila kabila lina utaratubu wake juu ya dawa asili za kuwapa watoto ili wapite kwenye zile hatua za ukuaji pasina matatizo yoyote hapa nazungumzia kukaa, kutambaa, kusimama, kutembea, kukimbia na kuota meno wakati mwingine kuchangamka.
Kwetu Tanga mtoto anapokuwa mchanga huoshwa na mavuo maalumu na kupewa dawa za kunywa za miti shamba ni miti ya aina saba na magome ya mti fulani na pia hupewa dawa za kunywa za miti minne maalum akitoka hapo km mtoto wakiume anakua mwanaume kweli kama wakikeanakuwa wakike kweli mliokutana na watu wa tanga mnanielewa zile shughuli zinaanza kupikwa utotoni.
Leo ntazungumzia kifua kwa watoto wadogo. Kifua kinaweza kusababishwa aisha mtoto kula uchafu wakati anazaliwa hii ni pumu. Lakini pia yaweza ikawa hali ya hewa na mambo mengine
Dawa zake nimezigawanya katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza watoto kuanzia mwaka siku moja hadi mwaka mmoja, sehemu pili kuanzia mwaka hadi miaka 5
Kwa watotot wa changa
Kwanga watakiwa umuangalie ana tatizo gani yaweza ikawa maziwa unayompa hayapendi, au vyakula anavyokula mzazi vinamuathiri pamoja na vingine ikiwa ni pumu subiri atimize mwaka mmoja
Kama ni mafua na kifu cha kawaida chukua punje kadhaa za vitunguu saumu zitwange ziwe laini kabisa kisha fuata taratibu zifuatazo kwa ufasaha
Mpake kweny unyayo wake mtoto kwenye kifua ila kifuani usimpake sana chukua mpake kiganja ambacho anapenda kukinyonya kidogo alafu jipake mzazi kwenye mikono umnusishe kwa mbali puani wakati unamnyonyesha paka juu ya maziwa yako sio kwenye chuchu anaponyonya
Wakati unamnyonyesha hakikisha ile alama nyeusi ya duara ya chuchu imeingia mdomoni mwake yote
Watoto juu ya mwaka
Tiba Yake, chukua majani ya mpera kiasi cha kama viganja vinne, yaponde pamoja na magome ya muembe 'ukipata mwembe tanga au dodo ni vizuri zaidi' kiasi cha viganja vinne,
na tunda la koma manga, twanga vyote kwa pamoja ( Yani majani ya mpera, magome ya muembe na tunda moja la komamanga ).
Ukisha maliza kutwanga, changanya na maji lita mbili halafu chemsha pamoja na lita moja ya asali mbichi ya nyuki wadogo.
Chemsha hadi itokote, halafu ipua dawa yako
Matumizi : Kwa mtoto mdogo mwenye umri wa kati ya mwaka mmoja na miaka mitano, tumia kumpa kijiko kimoja kikubwa mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni n kwa siku saba.
Hii hata kwa watu wazima wanaosumbuliwa na kifua hutumia vijiko viwili vya chakula mara mbili kwa siku ndani ya siku 21.
Wabillah tawfiq
www.tabibuasili.blogspot.com
Comments
Post a Comment