VITU VINAVYOLETA MVUTO WA WATEJA KWENYE BIASHARA YAKO



HII ni makala ya pili ambayo naitoa kuhusiana na masuala ya mvuto wa biashara. Leo nitagawa mafungu mawili ya biashara zile za kutembeza  na zile za kwenye frem.

Zakutembeza nazijumlisha na na wale wanaofanya biashara kwenye mitandao ni sawa tu na wale wanaotembeza. Hawa sasa jinsi kufanya ili biashara yako iwe na mvuto fuata maelezo yafuatayo.

Kwanza wewe mwenyewe uwe na mvuto bimaana usiwe na nuksi mikosi wala hasadi hapa inakupasa utumie dawa za mvuto kulingana na nyota yako ili kukupa mvuto zaid. Pili unatakiwa uwe na pete ya bahati ya nyota yako pia upate dawa za mwili bimaana kuchanja mpaka ulimi ili unapoongea na mtu avutiwe na kile unachokiongea na iwe rahisi kwake kutoa maamuzi.

Ukifanya hivyo utawachoka wateja sasa njia fupi yakukusaidia kwa haraka lakini c yakudumu koga maji ya bahari walau hata mara mbl kwa mwezi hakikisha iwe alhamisi saa sita uck au jmos saa nane wakati ukitoka choma udi au paka mafuta ya mvuto kulinganana na nyota yako.

Wale wenye biashara za frem pia halikadhalika watakiwa kuisafisha frem yako na kuweka dawa za kuita wateja pia na mwenyewe kujiweka mvuto kama nlvyoeleza hapo juu. Washa udi kila ufunguapo duka lako niliwah kueleza nguvu za udi na mshumaa kwenye group sasa utatumia udi.

Penda kupigia deki au mwaga  maji ya bahari walau mara mbili kwa mwez.

Epuka kuweka vitu vya kiza dukani epuka kujipamba mapambo ambayo hayaendani na nyota yako  nlishafafanua wiki hii kila nyota na rangi zake na mapambo nenda kasome 

Waweza tumia pilipili manga wengi huita pilipili mtama twanga upate unga wake mwaga sehemu yako ya biashara usiku wakati unafunga siku ya pili fagia huo unga na taka za dukani kwako kisha chimbia kishimo mbele ya duka lako fukia

Nzuri kama utamwaga alahamisi na utafagia ijumaa saa 12 kabla mchomozo wa jua
Watu wakishuka msikitini choma mwita na mchekea vnapatikana maduka ya dawa asili

Hizi ni rasha rasharasha kikubwa ni hicho nilichokufungua hapo juu tengeneza biashara yako.

Kama ni kwanza unaanza biashara basi fungua kwa dua na wape watoto sadaka
Mungu atakufungulia milango ya ridhk

Kwann nmezungumzia nyota, fahamu kuwa nyota ndo ufunguo wa kila kitu katika maisha yako ndiyo inayokuonesha mafanikio yako utayapata wapi katika mapenzi biashara nk


Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI