UKIOTA UMENG'OA MENO AU JINO KUDONDOKA NA FIDHI KUUMA NINI MAANA YAKE


HAPA NAONGELEA tafsiri za meno kung'oka na maumivu ya fidhi. Ndoto hzi zina maana kubwa sana kwa muotaji iwapo zifakujia mara kwa 

mara.

Kwa mfano wewe una maumivu ya meno na umeambiwa kesho wenda ng'oa jino usiku ukaota unag'oa jino ndoto hii haina tafsiri ni ubongo tu unakukumbusha kuwa kaa tayar kwa maumivu ya kesho.

Ndoto ninazo zitafairi hapa ni zile za kujirudia mara kwa mara na uotaji wake ni usiku mkubwa tafafhali soma kwa makini kisha ndo uulize swali ukiulza swali ambalo nmeshaliffafanua sitalijibu okoa muda

Tafsiri za meno kung'oka kila jino lina tafsiri yake kama unavyoona kwenye kinywa chako kuna meno ya juu meno ya chini meno mbele meno ya nyuma meno madogo na meno makubwa.

Ukiota jino la mbele la chini limeng'oka hasa katikati ni ishara ya migogoro katika ndoa na itapelekea kutalikiana yaani kuachana.

Ikiwa meno ya mbele yameng'oka na kusababisha maumivu na kutoka damu katika ndoto, inamaanisha kutokua na uwezo kufikia malengo yako pia Ikiwa yameanguka bila ya kuhisi maumivu au kutoka damu, yamaanisha kupoteza mali yako.

Ukiota meno ya mbele  yanavunjika si kung'oka utalipa deni lako kidogokidogo. Ukiota mtu meno yake yamerefuka na yamezd ukubwa ni dalili ya mijadala na uhasama utakaotokea nyumbani au mbilini,

Kung'oka meno yote katika ndoto

Ukiota umengoka meno yote na ukayaweka mkonon muotaji ataishi maisha marefu kuliko ndugu zako aliozaliwa nao na ataishi  mpaka meno yake yang'oke yote atakufa akiwa kibogoyo.

 Na ukiota meno yote  yamedondoka ardhini ni dalili ya umauti na huna umri mrefu kuliko nduguzo uliozaliwa nao.

Na ukiota meno yote yamedondoka na yakapotea machoni mwako ni dalili watu wa nyumbani kwako wote watakufa kabla yako,

Ukiota meno yote yameng'oka na yamedondokea mapajani mwake kunamaanisha kupata kizazi kingi.

Kuyaokota meno yaliyoanguka pia yamaanisha kusema kitu ambacho atajuta kwa nini alikisema. Pia Kuota unang'oa meno kwa ulimi ni dalili ya kuharibika mambo ya watu wa nyumbani kwako kutokana na maneno utayoyazungumza.

Mwanmke mjamzito akiota analitoa jino lake bila shida au maumivu yoyote ni ishara ya kujifungua mtoto wa kiume hii hata mume ukiota ni ishara ni hyo hyo. Na ukiota unagoa jino kwa shida fidhi kutoka damu ni ishara ya kujifungua kwa upareshen pia ni ishara ya kuiacha familia wakt wa kujifungua mtoto au mama.

Ikiwa mtu amepoteza meno yake na akapata shida katika kula, yamaanisha umasikini dhiki na maradhi yasiyopelekea kifo chake

Na akiota meno yamedondoka akayachukua kwa mkono au anayakusanya kwa ndevu katika mapaja yake ni dalili kuwa uzazi wake umekatika hatozaliwa kwake mtoto tena na akizaliwa mtoto hataishi mungu atulindie vizaz vyetu

Kila mmoja kwa nafasi yake amche mola wake. Ndoto hizi ukiota kulingana na tafsiri niliyotoa tafuta ufumbuzi kwa wataalam walio karibu nawe

Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI