IPI TAFSIRI YA KUOTA UNAKULA NYAMA UNALISHWA VTU NA UKAHISI HARUFU BAADA YA KUSHTUKA FAHAMU KWA UNDANI
NDOTO hutafsiriwa kulingana na mazingira ya muotaji pamoja na masaaa aliyoota. Hapa namaanisha si kila ndoto ina tafsiri na si kila ndoto ina tafsiri moja yategemea na mazingira ya muotaji yapoje mazingira ndio huleta tafsri halisi ya ndoto. Pia si kila mtu ana uwezo kutafsiri ndoto. Kutafsiri ni elimu na kipaji maalumu kutoka kwa allah. Leo tuangalie tafsiri ya kulishwa au kula vitu ndodtoni. Maisha ya mwanadamu chakula ndio kila kitu, mlo ndio uhai na maisha yenyewe. Ikitokea mtu hajakula chakula fulan muda mref kisha mchana wake ukaiwaza upo uwezekano mkubwa usiku kukiota hcho chakula ucku wake. Ukiota unakula nyama mwenyewe bimaana hulishwi tafsiri yake ni dalili ya kutaka mafanikio ama kufanikisha jambo lako kwa njia ya kudhuru ama kuumiza wengine, yaani ufanikiwe wewe lakini ukiacha wengine na madhara. Ili upate nyama lazima kiumbe kipoteze uhai wake, mfano kirekebisha nyota yako utakapochinjiwa kuku mweupe basi umetoa uhai wa kuku ili kuweka sawa yakwako ndio tafsir