UKIOTA UMEKUFA UKIOTA UNAONA MAITI NDOTO ZA VIFO NA MAZINGIRA YAKE ISHARA NA TAFSIRI 'NDOTO ZA VIFO EP 2'


Kama nilivyozungumza katika makala ya awali kifo ni mwisho wa mwanadamu na ni mwanzo wa maiti. Kwa hiyo ukiota kifo inaashiria ni mwisho wa jambo fulani na ni mwqnzo wa jambo jingine yweza ikawa kutoka kwenye ubaya kwenda kwenye wema au wema kwenda ubaya huzuni kwenda furaha umasiki kwenda utajiri na kinyume chake


  NDOTO ZINAZOHUSINA NA MUOTAJI KUFA

Ukiota umekufa kisha ukafufuka utafanya madhambi na utamuomba mungu msamaha kabla ya kifo chako. Au utafanya mabaya mengi ila utakuja kujutia kwa kile ulichokifanya. Pia uashiria biahara kesi ama jambo lilnalokukabilia litakusukumbua sana ila mwishowe utamaliza kwa usalama.

Pia kuota kufufua yaani ulikufa kisha ukafafuka na kuwa hai kama muotaji yupo katika hali ngumu kimaisha ama maombi ya jambo fulani ni ishara ya kuwa utaondokana na ufukara au kurejea mtu aliyekwenda mbali hapa zaidi yatizamwa mazingira ya ndoto na masaa aliyootoa muotaji na hali aliyokuwanayo wakati huo.

ukiota umezikwa Ishara ya kuishi muda mfupi na utakufa bila kufanya toba. Ila ukiota umekufa ghafla bila kuumwa na hakuna tukio la mazishi utaishi umri mrefu. Pia kwa watafutaji huashiria hali isiyokuwa njema unaweza kutapeliwa ama kutolipwa amana unayodai hivyo yakupasa utumie nguvu za ziada. Pia wakati mwingine huashiria safari ya mbali isiyokuwa na marejeo yaan kama muotaji ni mtu wa safar au alikuwa anasubr safar kisha akaota kazikwa kuna ishara ya safari ya mbali.

 Ukiota umekufa kisha hukuzikwa ila watu wapo kwenye mipango ya mazishi ila ndoto ikaishia kwenye mipango ya mazisihi ukashtuka. Huashiria dunia yako itakuwa nzuri lakini akhera yako imeharibika. Pia huashiria kuna mambo unayafanya mabaya itakuwa kuwakost nduguzo yaan unaweza sababisha matatzo ukakimbia mji kisha kazi ukaichia familia yako.

Ukiota umekufa watoto wako na mkeo ndio wanaokuandaa kwa ajili ya mazishi pia haina tofaut huashiria utatafuta majanga na utawaachia watoto na mkeo majanga. Hovyo wakumbushwa uwe makini katika matafutaji yako na harakati zako. Pia ukiota umevishwa sanda wewe mwenyewe nii ishara ya kifo chako hivyo jibiidishe kufanya ibada kuwaomba radhi uliowakosea wakati mwingine huashiria mabalaa kwako.

             NDOTO ZINAZOHUSU MAITI

ukiona maiti inajisha yenyewe ni ishara ya watu wako watatoka kwenye majonzi na mali yao itazidi. Kama kuna mgonjwa atapona kama mnadai mtalipwa kama mwadaiwa mtalipa. Pia hushairia vita ama uaudi unautafuta mwenyewe. Wakati mwingine hufasili maisha ya huyo mtu uliyemuota anajiosha bimaana kuna jambo baya kwake litamkuta ama atalisababisha ila atapambana nalo mwenyewe hatahitaji msaada wa mtu. Ila halitakuwa jambo jema lazma litaacha makovu ya maumivu kwa watu.

ukiota maiti imevishwa sanda ila haijaenea mwili mzima utatiwa kwenye majaribu mazito ya zinaa na mtu wako wa karibu  lakini hutokubali. Ukiota umeona sanda pekee ni ishara ya zinaa inakuja mbele yako ukimuota mkeo mumeo anavishwa sanda na haijakamilika jua ana mipango ya kuzini au ana zini. Hapa tuliza kichwa chako kuna kuiona maiti inavishwa sanda kuna kuiona sanda pekee pia kuna mke mume mpenzi.

Ikitokea kwenye ndoto mmebeba maiti mwenda nayo sehemu kisha maiti ikaamka kuwakimbiza ama ikaanza kuwatisha ama ikawanasia ishara ya mipango yenu ya haram mnayoifanya haina mwisho mwema hivyo mwatakiwa kuongeza umakini ama kuacha hayo mambo ya siri. Ikitokea umeibeba maiti unaenda nayo sehemu inayojulikana kama sokoni hushiria faida ya mali na bishara zako zilizkwama zinaweza kupata ahuen.

Ikiwa utaota unaifufua maiti ama kuisadia jambo lolote maiti inaashiria utamsilimisha mtu wa dini nyingine au mtu muovu atatubia dhambi zake kwako. Au utaweza kuwashauri watu waovu kuachana na mambo ya kidhalimu wanayofanya.

Ukiota umehifadhi maiti ndani kwako ama sehemu yako ya biahsra ikiwa ya mtu unayemjua hutafsriwa uhhsiano wenu na huyo mtu. Ikiwa maiti usiyoijua huashiria utaletewa ama kuingiza vitu vya harama eneo uliloota. Kama utaingiza mwwnyewe inaashiria wewe mwenyewe ndiyo utashiriku uovu ama dhambi ikiwa utaikuta maiti ndani na imevishwa sanda ishara ya usaliti unaoendelea ndani kwako yaweza kuwa mapenzi ama mambo ya kifamilia.

Ikiwa utaota maiti ipo ndani kwako uchi ishara ya kuzalilika kwa maovu unayoyafanya hivyo uongeze umakini. Ukiota unaitoa maiti ya mtu usiomjua nyumban kwako ishara ya kujiondoa ama kujikwamua kwwnye mitihani ikiwa.

MAITI YA MTU UNAYEIJUA HUTAFSURIWA UHUSIANO WENU NA MAZINGIRA YA NDOTO. MAITI USIYOIJUA HUTAFSIRIWA KAMA NILIVYOELZA HIVYO UTAANGALIA MAELEZO YANAYOENDANA NA NDOTO YAKO UKIONA VINAPISHANA UKIZA HAPO CHINI UTAJIBIWA PASINA SHAKA YOYOTE

SOMO LIJALO TUTAONGELEA KUHUSIANA NA MAJENEZA NDOTONI NA MAKABURI HUASHIRIA NINI USISITE KUTOA SHUKRAN YAKO KWAN NENO SHUKRAN PIA NI SADAKA TOSHA NA KUONESHA TUNAENDA PAMOJA. SWALI LOLOTE LA NDOTO LIULIZWE HAPA CHINI NITALIJIB INBOX GHARAMA YA KUTAFSR NDOTO NI ELF TATU

Kama umelielewa somo  pia waweza shea na wenzio

Kwa wenye matatizo maalumu ya afya. Nyota kazi mapenzi kuibiwa nguvu za kiume uzazi kukuza snk niachie ujumbe inbox kwa wanaohitaji msaada wa dawa na tiba +255621442936

JiTAHIDI KUPIGA SIMU IKIWA UNATUMA UJUMBE BASI WEKA MAELZO YA KUTOSHA JINA PAHALA ULIPO NASHIDA HUSIKA JUMNE FUPI HI MAMBO NIAJE HABAR NK SITAZIJIB

Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI