FAHAMU KUHUSU MAFUTA YA MCHAICHAI FAIDA NA MATUMIZI YAKE

MCHAICHAI MMEA NA MAFUTA YAKE TIBA KWA MARADHI YA UREMBO ASILI.

NILIWAHI kuongelea kuhusu mchaichai kwa urefu jinisi inavyotibu maradhi mbalimbali na kuhusu masuala ya mapenzi kama ilikupita itafute kupitia page yangu ya mtabibu asili tz.

Leonitaongelea faida za mafuta pamoja na mchaichai wenyewe. Asili ya mchaichai ni bara la Asia hasa nchi za falme za kiarabu. Mafuta yake asili hutokea huko Asia kwan ndiyo wenye ujuzi wa kuyandaa vzur.

Mafuta ya mchaichai yana faida nyingi sana kwa maradhi ya ngozi na urembo wa wanawake. Ukichukua mafuta ya mchaichai ukachanganya na mafuta ya zaituni 'oliv oil' ukipaka kwwnye nywele utazifanya kuwa nyeusi kuondoa mba kujaza nywele. Huondoa mabaka kichwan kwa watoto hhondoa mapunye sugu. Huondoa utangotango matumizi ni kupaka sehemu iliyoathirika.

Ukichukua mafuta ya mchaichai ukachanganya na mafuta ya nazi ni dawa nzur ya maumivu ya kufanyia massage mwili mzima. Ni mafuta mazur kwa watoto wadogo. Kwa maumivu ya miguu kuwaka moto kufa ganzi chukua mafuta ya mchaichai changanya na mafuta nyonyo olive oil weka na alymit tumia kuchua.

Kwa maumivu ya kioanda uso na kichwa chukua mafuta chua kwwnye paji la uso maumivu yatakata

Tiba ya sukari ya kupanda majani mchaichai huchemshwa katika maji kisha maji hayo kiasi cha kikombe kimoja cha chai yatiwe unga wa tangawizi kiasi cha vijiko 2 vidogo. Mgonjwa anywe maji hayo kiasi cha kikombe 1 asubuhi kabla kula kitu chochote na jioni kabla ya chakula cha usiku .Tiba hii itumike kila kwa muda wa mwezi mmoja.

Vidonda vya tumbo chemsha majani mchaichsi kiasi cha nusu lita,mgonnjwa anywe maji hayo kiasi cha kikombe kimoja asubuhi na usiku kabla ya kulala.

Kama un tatzo la kuota mapele umalizapo kungoa tumia mafuta ya mchaichai kama aftershave yako hutaona tena mapele

Tumia mafuta kupigia deki ndan kwako au dukan kwako, pia waweza changanya na mafuta yako ya kupakaa huleta nuru ya uso.

Pia hutumika kutengeneza uke kuongeza ashki la tendo la ndoa pia huongeza mapenzi, lakini pia mafuta yake wahenga waliyatumia kwa mahitaji ya kutimiziwa haja zao yaani kama mtu akusikilizi haya nitayafafanua kwenye group la whatsap.

Kuhusu mchaichai unapatikana maeneo mnayoishi mafuta yake uanapatikana maduka ya dawa asili na vyoye nlivyotaja ila mafuta kuwa makini mengi siku hz yanachakuliwa kwahyo unaweza ukashindwa kupata matokeo haraka.



Link ya group la whatsap hii hapa utakapoingia uliza 

https://chat.whatsapp.com/FliiJufC9CpCcr0qnmMDh6

Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI