FAHAMU UKWELI KUHUSU KUBEMENDA MTOTO DAWA NA KUJIKINGA KWAKE



JANA niliuliza swali kihusiana na kubemenda mtoto. Nilihoji nione ufahamu upoje miomgoni mwetu. Nilipata majibu tofaut yanayokinzana hapa nitayaweka mafungu matatu. Kundi la kwanza wamesema hawajui ila wanasikia tu. Kundi la pili wanauelewa lakini wanakinzana wapo wanaosema hutokana na jimai ya nje ya ndoa lakini wapo wanaosema ni jimai ya ndnai ya ndoa. Kundi la mwisho wao hawaamini kwenye jimai bimaana jasho linalotokana na tendo la ndoa wanaamni kwenye sayansi lishe, soma ufafanuz zaid anayekuletea uchambuzi huu ni Mtabibu ASILI TZ.


Muda mrefu pengine tangu kuzaliwa kwangu hili neno la kubemenda sio ngeni masikioni mwangu. Wakati nakua nilkuwa sifahamu zaid kuhusiana na neno lenyewe lakini pia kinacholeta ili hili neno litumike. Leo nitakupa nitachambua kuhusu kubemenda kiundani zaidi. Kwanzq tuanze neno lenyewe kubemenda ni kitendo cha mtoto kuvia yaani kurudi nyuma katika makuzi yake. Mfano mtoto alikuwa kwenye hatua ya kutembea ukimbemenda anarud kwenye kutambaa yaan haend mbele anarud nyuma.

Kuna sayansi zinasema mtoto akikosa lishe iliyobora husababishwa kubemendeka. Sababu unayoitoa ni kwamba mwili unakuwa haujijengi kimakuzaji ya mtoto hivyo mtoto huvia hudumaa. Wakaenda mbali zaid wanasema ili mtoto apate afya na makuaji mazuri lazima uwe na mfumo mzuri wa kumpangia mlo ulio kamili na unaoendana na rika lake. Huu ndio uchambuzi wa kisayanzi japo sitaki kubishana nao sana lakini kuna tofaut kati ya mtoto kudumaa na kubemendeka nitaeleza mwishoni mwa makala haya.

Wanasayans huwa hawaamini sana kwenye mambo ya kiimani ukisoma biblia na kuruan mtu wa kwwnza kuumbwa na ADAM NA HAWA au EVA ila sayansi inakataa hili. Kwa hiyo hata kwenye kubemenda kuna ukaksi ndani yake. 

Ukweli wenyewe kuhusu kubemenda ni kwamba ni lile jasho ama uchafu unaotokana na kufanya jimai tendo la ndoa kisha likamkuta mtoto ambaye bado mwili wake haujatengemaa. Hapa tuwe makini kidogo kwenye kusoma uchambuzi na maelezo. Mtoto anabemendwa na baba na mama yake kwa kutoka nje ya ndoa, au mama kubeba mimba wakati ana mnyonyesha mtoto.

Ikitokea baba au mama kaenda kufanya jimai nje isiyo halali yake na akaja akamshika mtoto pasipo kujitwayarisha mtoto huyo anabemendeka. Yaan ninakizungumzia umetoka nje ya ndoa au mahusiano yako ukaenda kufanya mapenz na mtu mwingine kisha ukarud pasina kujitwayarisha ukimshika mtoto unamuharibu.

Mama na baba halali ikitokea wamekutana kiwmili mwatakiwa mkaoge kwwnzw kabla ya kumshika mtoto. Yaan ikiwa mmetoka kifanya mapenzi kaogeni kwanza kabla ya kumshika mtoto hata kama akiwa yualia.hii itamupusha na hilo jasho lenu.

Ikitokea mama akaenda kukutana na mtu ambaye si baba wa mtoto kisha akamimina manii yake ndani ya uke mama huyu hata kama ataenda kuoga mtoto akinyonya yale maziwa ya mama anaweza kuharibika kwa sababu mtoto amekula vtu ambavyo hana unasaba navyo.

Ikiwa mama akibeba mimba na ana mtoto anayonyesha basi haruhusiki kumnyonyeha mtoto atakiwa amuachishe hata kama ana miez minne. Kumnyonyesha kunaweza kusababisha kumbemenda mtoto.

Ukiachana na masuala ya jimai kuna uchawi mtoto akifanyiwa huonekana kama aliyebemendwa na hii ni mbaya zaid kuliko huko kumbemenda. Wachwai humlisha unga wa mifupa za maiti za watoto ambayo humnyong'onyesha na kumdhoofisha makuzi yake. Hapa pia kuna mazongo wale ndugu zangu wa Handen Lushoto KwaMgwe wanafahamu zaid haya mambo mtu ikipogwa zongo unakuwa kama mlenda vile.

Dalili za mtoto aliyebemendwa. Ni kukatisha na kurud nyuma ukuaji hatambai wala hasimami kakaa tu. Anahara 'kuharisha' au kujisaidia kila mara. Anadhoofu kiafya na hata muonekano wake unabadilika. Mtoto mwenye mazongo anakuwa na dalili hzo kisha tumbo humuuma zaid au kujaa macho kupoteza ile mboni.

Sasa mtoto aliyedumaa yeye anakuwa hakui kimpangailio anakuwa ila hakui kama wenzio anawwza akatoka kitumbo ana akazidi kuwq mfupi na pia hata uelewa wake huwa mdogo na hii huwapata waoto ambao washaaanza kutmbea sababu kwetu hasa vijijini watoto wanakua kwa kula uji wa bada 'unga wa muhogo' na hakuna shida yoyote.

Ikiwa umebemenda mtoto kuna madawa mengi yapo makombe zipo dawa za kuwekwa kwenye uji ipo mizizi kuchemsha. Dawa nyepese kuna mti unaitwa mlangamia au mtetkuwanga au mfungafunga nishauzuzngumzi mara kadhaa kuona picha angalia makala zilizzopia una asili ya kuota juu ya mti mwingine una asili ya kambakamba. Hauma matawi unatoa vitunda vidogo.

Achemshiwe hizo kamba na mama yake anyweshe kisha kamba zingine ziweke kwenye beseni baba na mama wazifikiche kwa mikono yao kisha aogeshwe mtoto

Nmefafanua kwa upana kisayansi, na uhalisia wenyewe wa kubemenda mtoto. Nmewah kuzungumza kwamba watoto wakizaliwa kuna mavuo huoheshwa ili kuepukana na mambo kama haya pia kumchangamsha mtoto. Mavuo ni madawa maamulu mchanganyo wa miti na magome huchemsha na kuogeshwa na kunyeshwa motot. Hizo ndizo kinga

Una tatzo lolote la uzazi, kazi, nyota, nguvu za kiume, kukuza dhakar, biahsra mapenzi nk niachie ujumbe inbox

+255621442936

Whatsp group ni la malipo

Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI