FAHAMU KUHUS NGIRI, CHANGO NA MCHANGO KWA WATOTO NA TIBA ZAKE

NGIRI, CHANGO NA MCHANGO KWA WATOTO

UHALI gani mpenzi mfuatiliaji wa ukurasa wa Mtabibu ASILI TZ. Leo tutazungumzia kuhusiana na ngiri kwa wanaume chango kwa waanawake lakini kwa watoto huitwa mchango. Kiuhalisia ni magonjwa yanayoshabihiana hutofautisha umri na jinisa tu. Ikiwa hujakuwa makini kumtibia mtoto basi anapokuwa mkubwa huja kumsumbua. Pia kuna kipindi husumbuliwa akiwa mtoto lakini kadri anavyokua ugonjwa hupotea.

Ngiri na chango hujitokeza baada ya balahe kwa msichana pale anapoanza kuona siku zake ndipo maradhi haya huanza kujiyokeza maana huwenda sambamba na mfumo wa uzazi. Kwa mwanaume pale anapoanza kuzalisha mbegu za kiume ndipo hujiyokeza maradhi haya. Wapo wanaorithi ikiwa ukoo wako unaaslili ya magonjwa haya basi kunabuwezekano mkubwa kuupata ni kama pumu vile.

Ngiri kuna utofaut kuna ngiri ya kawaida ambayo hukubana wakat wa bard kali tumbo kuunguruma kende moja kushuka na kusinyaa hujikuta mtu amejikunja hawez kujikunjua mpaka imuachie. Na kuna Ngiri maji ile ya kujaza maji kende au kwa lugha nyepeai huitwa mshipa. Huu mshiba unatibika kwa dawa za asili ikiwa utauwahi kabla haujakuchosha sana matibabu yake ni kitaalam zaid siwez kuyaandika hapa.

Kuhusu ngiri pale inapokubana unaweza tafuta mizizi ya mturatura au ndurere ukachanganya na mizizi ya mkunde pori au muinga jini ukachemsha ukanywa na kuchua kwenye makende na upande wa tumbo inakuachia mara moja na utaendelea na shughuli zako. Au unaweza kunywa mafuta ya habbat souda au kuramba unga wa habbatsouda, ikiwa ni unga utachanganya na asali kidogo. Kuna dawa ukitaka kutibia kabisa tatzo utapatiwa.
mturatura au ndulelel

Chango lina tabia ya kubana wakati ukiwa hedhi tumbo linanguruma sehem ya haja kubwa kuhisi kama unachomwa na misumari huwez kushika mimba ukiingiliwa maumivu hizo ni baadhi ya alama za chango linatibika kwa kupikiwa madawa wengine huchanganya na kuku jike au nyama ya mbuzi. Pale unapobanwa na chango tafuta majani ya mpatakuva yachemshe kunywa kikombe kidogo mara tatu kwa siku. Pua hyo nilioelekeza kwa wanaume unaweza itumia. Pia ukipata mizizi ya kikulagembe pia inatumika kwa tumbo la chango. 

mkunde pori

Kwa watoto wa kike wanakuwa na mngurumo wa tumbo wa kiume pia wananguruma tumbo vikende vyao au uume vinasinyaa na kuingia ndani wakati mwingine mwili huota vipele vidogodogo na kuwashwa huo ndip mchango kwa watoto. Ukiwa na mtoto mwenye ugonjwa huu yatakiwa uwe mafuta ya habbat souda nyumban kwako utakuwa unamlisha pale unaposikia mngurumo tumbon kijiko kile kidogo tena utaweka nusu.
mafuta ya habbat souda

Pili kwa watoto wa kiume utafute mpapai dume ule uisozaa unatoa maua tu chukua mizizi minne kisha upate na mizizi mitatu ya mtura kamba utymie ya mgomba kuzifunga hiyo mzizi iwe mzigo mmoja utachemsha utampa vijiko viwil vidogo mara tatu kwa siku kwa watoto waliopitisha mwaka na nusu chini ya hapo ni kijiko kimoja. Kwa watoto wa kike utachukua mizizi saba ya mkunde pori ndio huo muinga jini utachemsha matumizi na kuifunga kama nilivyoeleza hapo juu.
mpapai dume

Sasa akiwa na vipele atakiwa apate na dawa za kuoga utachukua majani ya mvuje utachanganya na majan ya muinga jini na mpatakuva utachemsha utamchanganyia kwenye maji yake ya kuoga utamuogesha kwa siku saba mara mbili kwa siku.

Nmeeleza kuhsu ngiri chango na mchango wa watoto madawa niliyoyataja hiyo miti inapatiakana majumbananapoishi hayo mafuta utayapata maduka ya dawa asili. Mimi natoa dawa za kutibu zilizotayar.

Maswali uliza hapo chini ruhsa kushea usikop

Una tatzo lolote la pumu, nguvu za kiume, bawasiri, biashara, uzazi, kazi, mapenzi nk niachie ujumbe inbox

+255621442936

Whatsp group ni la kulpia

Comments

  1. Mm pia nataka hiyo dawa y shango

    ReplyDelete
  2. Mimi mwanangu huwa anahivyo vipelewa na vinamrudia Mara kwa Mara nataka nimtafutie hiyo dawa ya kunywa na kuoga sasa majina ya hiyo dawa mvuje,mpatakuva na mjinga jini ndo zipojee au kwa majina mengine zinaitwajee

    ReplyDelete
  3. mtoto wangu anasumbuliwa na tumbo linakuwa linammbana anashtuka kama kaa kwenye kiti anaweza dondoka

    ReplyDelete
  4. Je chango huleta degedege maana mm Nina mwanangu anamiaka 9 ni WA kike naambiwa ni chango

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI