KUHUSU NYOTA MAFANIKIO, MAPENZI SIKU NA SAA ZA BAHATI ' NYOTA YA KAA'



MUENDELEZO wa maandiko yanayohusiana na uchambuzi wq nyota, na hiimakala ya nne katika mfulizo wa makala 12 za nyota ambazo nimepanga kuzizungumzia hapa na leo tutazungumzia nyota ya KAA. Tutagusia mafanikio siku za bahati namba za bahat na tabia zake katika mapenzi anayekuletea darasa hizi ni Mtabibi ASILI TZ.


Hii ni nyota ya nne kwa uzawa katika nyota 12 watu wa nyota hii ni wale waliozalia kuanzia tarahe 21 Juni mpaka 22  Julai. Hapa namaanishia waliozaliwa kunazia tarahe 21,22,23,24 mpaka mwezi jui unapoishia na tarhe 1,2,3,4 mpaka kufikia tarahe 22 mwez julai wote nyota yao ni KAA. Ikiwa hujui tarahe yako ya kuzaliwa  kama una jina linaanzia heruf D na H wote nyota yao ni moja.

Ikiwa unajua tarahe yako achana na kushughulika na jina tarahe ya uzawa ndio nyota yenyewe ikiwa hufahamu ndo angalia herufi ya jina lako. Narejea tena nyota ni tarahe ya kuzaliwa ukiwa hufahamu tarehe ndio uangalie heruf ya jina lako.

       ASILI RANGI SIKU NA SAA ZA BAHATI ZA KAA

Asili ya nyota hii ni maji sayari yao ni Mwezi, siku  yao ya bahat ni Jumatatu, namba zao za bahat ni 2 na 7. Malaika ya nyota hii ni Jibril, jini wao katika nyota hii ni Nuuril Abyadh.

Pete zao ni za fedha viwe vito vya lulu, Moonstone, Almas, Peacock yategemea na hitaji la mtu ahitaji kwa shughuli gani. Manukato yao ni Jasmine na Sandalwood. Mafusho yao ni ubani wa aina yoyote wachome siku yao ya bahati.

Vyakula vya nyota hii nia vyote vya kutoka baharini ikiwemo kaa wenyewe na samaki mboga zao kabichi na saladi matunda yao ni mapeasi

Rangi zao ni Nyeupe, Bluu, Hudhurungi (Puce) na rangi ya Fedha (Silver), Wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi zozote ambazo siyo nzito au zenye uwiano na rangi nyeupe.

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Nyeusi(Black) na Bluu iliyoiva (Indigo).

Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni rangi ya Machungwa na rangi ya Dhahabu.

Watu wa nyota hii asili yao ni ungozi, ving'ang'anizi. Wana hisia na wanapenda kulea au kulelewa. Wanapenda sana familia na nyumba zilizopoa kwa amani na maelewano.

 

       NYOTA YA KUSHIRIKIANA NAE

Nyota ambazo atakiwa ashirikiane nazo ni Samaki na Nge, Nyota ambazo haziendan nazo ni Punda, Mizani na Mbuzi. Nyota inayomsaidia katika mapenzi na ushirkiano wa kifedha ni nyota ya Mbuzi. Msaada kikazi ni nyota ya Punda. Ushauri wa kihisia ni nyota ya Mizani. Msaada wa kipesa ni nyota ya Simba. Msaada wa ubunifu ni Nge. Msaada kidini ni nyota ya Mapacha na samaki.

Ukihitaji mtu wa kutumia nae ni nyota ya Nge,
Jiepushe na punguza kuwa na hisia kali na kung'ung'unika na kusikitika sehemu ambayo haipaswi manung'uniko.

       TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Kaa ni watu wenye tabia ya hisia nzito, wapole na wenye huruma. Ni wenye dhamira ya ulezi na kuwaangalia au kuwahurumia watu wengine, hiyo inaonekana waziwazi katika nyumba zao na familia zao.

Upande mwingine ni watu ambao wana “Gubu,” wakali, wenye kupenda kujishughulisha na wanajiamini sana. Ni watu ambao wanaweza kubadilika lakini wenye msimamo na itikadi, wanaweza kuwa ni wenye wivu mkali na wenye kupenda kudhibiti wapenzi wao.

Hisia ni kitu muhimu sana katika mapenzi kwa Kaa, pamoja na kwamba kimaumbile ni watu wanaopenda kujilinda na wanaogopa sana kuumizwa kimapenzi na wapenzi wao.
Wanapenda sana kuwa karibu na wanayempenda na kuwaonyesha huba na upendo mkubwa. Kwao hakuna mapenzi ya nusu nusu, wanapenda sana kuwa na mtu ambaye atadumu nae milele.

Kaa bila ya kuwa na mpenzi hujihisi hawajatimiza lengo lao katika maisha, hivyo basi huwa hawana raha. Ni wapenzi waaminifu na wanategemea wapenzi nao wawe waaminifu kama wao.Ni wagumu sana kuachana na wapenzi na inapotokea huwa hawaagi, wako radhi wao waumie kuliko kuachana na anayempenda.

             VIPAJI KAZI NA BIASHARA ZA KAA:
Kaa,Wanatakiwa wafanye kazi za Utabibu kama vile Madaktari au Wauguzi, kazi za baharini kama vile mabaharia, kazi za huduma ya chakula kama hoteli, migahawa, kazi za kuhudumia watoto kama katika shule za chekechea, kazi za benki au kazi za maneja utumishi au kazi za kuandika.

Kaa wana kipaji cha hisia ya kugundua mambo yanayotendeka ikiwa ni pamoja na kubashiri mambo, kumwelewa mtu kwa undani na kujua jambo ambalo mtu anataka kulifanya au jambo litakalotendeka hasa kwenye watu wengi.

            MAGONJWA YA KAA:
Nyota hii inatawala njia kuu ya chakula kuelekea tumboni, mbavu, mfupa wa kidari, tumbo la uzazi, utumbo mdogo na utumbo au sehemu zote za kusagia chakula.Vile vile inatawala bandana na matiti.
Maradhi yao makubwa yanakuwa maradhi yanayosababishwa na gesi, vidonda vya tumbo au kiungulia au maradhi yanayotokana na mwili kuwa mnene au umbo kubwa.

     MAMBO MUHIMU YAKUZINGATIA

Nyota inatafsiriwa kwa tarahe yako ya uzawa. Saa yako uliyozaliwa, ikiwa hujui tarahe ndio utumie heruf ya jina lako. Ikiwa nyota yako sijaizunguzumiza subiro makala zijazo unahitaji uchambuzi private utalpia gharama.

Una tatzo lolote la kazi nyota mapenzi biashara kesi kuuza nk niachie ujumbe inbox

+255621442936

whatp grouo n la malipo kwa wanaohtaj

Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI