UCHAMBUZI WA NYOTA RANGI, SIKU, PETE ZA BAHATI, MAFANIKIO NA MAPENZI 'NYOTA YA MASHUKE'



KARIBU tena katika muendelezo wa darasa zangu zinazohusiana na nyota, ndoto, miti shamba na dawa asili kwa ujumla. Leo tutazungumza kuhusiana na nyota ya Mashuke uchambuzi siku ya bahati rangi gani nzuri kwao namba zao za bahat na mambo mengine anaykuletea darasa hizi ni Mtabibu ASILI TZ.

Nyota hii ni ya sita katia ya zile nyota 12 za uzawa. Watu wa nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarahe 22 Agost hadi 22 Septembea. Ufafanuzi hapa namaanisha wote waliozaliwa kuanzia tarahe 22, 23,24,25, nakuendelea mpaka mwisho wa mwezi na wale waliozaliwa kuanzia tarhe 1,2,3,4,5 mpaka tarhe 22 mwez Septemba wote nyota yao ni Mashuke. Kama hujui tarahe yako wale majina yao yanayoanziwa na heruf P,T na R.


    ASILI RANGI NAMBA SIKU NA PETE ZA BAHAT

Asili ya nyota hii ni Udongo, Sayari yao ni Uttwarid. Malaika wao ni Mikyail jini wao anaitea Barkaan. Siku yake ya bahati ni Jumatano namba yai ya bahati ni 5.

Rangi za o za bahati ni Udongo, Njano na rangi ya Machungwa. Kama ukipata bahat ya kunua gar au kujenge nyumba basi rangi nyeupe ndio kivutio na itakupa nguvu katika umiliki wa hivyo vitu. Kwenye masuala au mialiko ya kimapenzi tumia rangi ya Bluu.

Pete za nyota hii ziwe na vito cha Almasi, Sugilite, Quartz na Peridot, green sapphire Manukato yao ni Mrujuani, mafusho yao ni Kachiri 'kashuu Muhlib' muda wa kuchoma kama una dawa ndio uchanganye na hayo mafusho siku ya Jumatano saa 12 asubuhi au saa saba mchana

Mashuke wanatakiwa kuvaa Nguo zenye Mitindo ya kisanii, nguo ziwe Nyepesi na zilizonyooka Ziwe za Rangi ya Njano na Nyeupe. Kitambaa kiwe kama hariri, chepesi na chenye kumeremeta. Wake kwa waume wapendelee kuvaa Suti na ikiwezekana wasikose kuvaa Gloves

Vyakula vya nyota nyota hii  ni kuku uduvi na karoti.

      NYOTA YA KUSHIRIKIANA NAYO

Nyota zinazoelewana nazo ni Ng'ombe na Mbuzi, nyota inayomsaidia kikazi ni Mapacha, msaada kihisia ni Mshale. Msaada wa kipesa ni Mizani, msaada kiubunifu ni Mbuzi.

Nyota inayombeba katika masuala ya mapenzi ushirikiano wa kibiashafa ni nyota ya Samaki. Nyota ya kutumia na kuonjoi nayo ni Mbuzi. Ukihitaji msaada wa mambo ya kidini na kiroho mtafute nyota ya Simba.

   ASILI YA TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Mashuke ni watu ambao wanaopenda kusoma. Wana akili nzuri ambayo inatumika zaidi katika kupambanua njia ya asili ya mpangilio wa mambo. Kwa ujumla ni watu ambao wanapenda kufuata kanuni na kufanya mambo kwa usahihi kabisa. Ni waangalifu sana hasa katika mambo madogo madogo na wanapenda kushutumu hasa mambo yanapokwenda vibaya. Wanatabia ya kuchunguza mambo na kuhakikisha mpangilio unafuatwa kikamilifu. Wanajituma na kujishughulisha na wanapenda sana kufuata sheria au mpangilio maalum ulioainishwa.
Katika Mapenzi ni watu wenye aibu kwa undani lakini wanajiamini, wanapokuwa katika mapenzi hunawiri.

Ni watu ambao inawawia vigumu kuonyesha penzi lao. wana mtizamo wa kufikiri kabla ya kujitumbukiza ndani ya penzi lolote, wanachunguza kwa makini matokeo ya penzi lenyewe. Wanapotafuta mpenzi wanaweza wakakupumbaza na maneno matamu na raha zisizo na kifani.

Ni vizuri kufikiria mara mbili kabla hujajiingiza katika mapenzi na Mashuke. Inawawia vigumu wao kukuanza wewe kimapenzi kwa sababu wana uhakika kwamba watashindwa. Kinachowasaidia ni subira na kuwaelewa wapenzi wao ndio maana mapenzi yanakua. Mara wakishapata mpenzi wa kweli wanakuwa waaminifu sana na watafanya kila njia kuhakikisha mapenzi yanakuwa hai na yenye kupendeza.

Hata hivyo wanaweza kuwa wasumbufu, wenye kulalamika na wenye mtizamo wa makosa ya mpenzi wake ili amshutumu. Kwa sababu ya hali yao hii mara kwa mara kunakuwa na ugomvi wa wapenzi ambao wanataka kutekeleza malengo yao.

Sifa ya Nyota hii ni wanakuwa na uwezo wa kubadilika badilika.Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye uwezo kuangalia mambo kwa mtizamo mkubwa zaidi.Maadili yao ni Uchambuzi, Wepesi wa Akili, Uwezo wa kuwa makini na Uwezo wa Kuponya.

  KIPAJI KAZI NA BIASHARA YA MASHUKE

Kazi zao ni uchapishaji, Utangazaji, Afya, Udaktari, Kazi za Unesi. Ualimu au ufundishaji jambo fulani. Shughuli za Uongozi Ukatibu na kazi zinazohusiana hasa na utendaji. Biashara yoyote ya kutembea au kukaa waweza ifanya.

Vipaji vyao ni kuhisi, kufikiri, kutambua tatizo au ugonjwa au kupata picha ya wazi akilini ya kutambua jambo lolote. Vilevile wana uwezo wa kuponya na wana uwezo wa kusoma michoro yeyote

Mashuke ni tegemezi, wenye bidii ya kazi na tabia ya kufanya kazi bila ya kuchoka. Wanapenda sana kazi zenye mpangilio na ambazo kila kitu kiko katika mpangilio maalum.Wanapenda kuwa huru katika kazi zao na kujitosheleza katika kila wanachokifanya, hufurahi kufanya kazi bila ya kusimamiwa.

MAMBO YA MUHIMU YA KUZINGATIA

Watu wa nyota hii wanaandamwa na maradhii ya utumbo, sehemu ya uvunguni mwa utumbo na neva zote zilizo chini ya kitovu.Kutokana na asili hiyo wale wenye nyota hii huwa wanapata sana matatizo ya maradhi ya ugonjwa wa tumbo au tumbo la uzazi au matatizo ya kizazi.Magonjwa ya mwili kushindwa kusaga chakula tumboni au magonjwa ya kujikunja utumbo na maambukizo ya utumbo.

Nyota inatafsiriwa na tarahe yako ya kuzaliwa iwapo huijui tarahe yako ndio uangalie herufi ya jina lako.

Maswali kuhusu nyota yaulizwe hapo chini. Soma makala zilizopita kuona nyota ambazo tayar zishafafanuliwa au endelea kufuatilia darassa zijazo kwa nyota zilizobaki. Uchambuzo wa nyota private utachangia gharama.

Una tatzo lolote la uzazi, nguvu za kiume, kukuz dhakar, biashara mapenzi kesi kuobiwa kuuza nk niachie ujumbe inbox 

+255621442936

Whatsp group ni la malpo kwa wahtaj

Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI