UCHAMUBUZI WA NYOTA SIKU, RANGI NA PETE ZA BAHAT, MAFANIKIO NA MAPENZI 'NYOTA YA NG'E'



KaRIBU tena katika muendelezo wa makala za uchambuzi wa nyota zenu, ikowa nyota yako tayar tushaizungumzia kuwa  na subira tumalizane na nyota za wenzio. Ikiwa nyota yako imeshapita nahukuiona angalia makala zilizopita kwenye ukurasa huu. Leo tunaendelea na makala ya nane ya uchambuzi wa nyota tukizuungumzia nyota ya Ng'e katika mafanikio, mapenzi, namba za bahati siku za bahati na pete zao aanayekuleata darasa hizi ni Mtabibu ASILI TZ.

Hii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Oktoba na 22 Novemba. Ufafanuzi hapa nawajumuisha wote waliozliwa kuanzia tarahe 22,23,24,25 na kuendelea mpaka mwisho wa mwez Octoba na kuanzia tarehe 1,2,3,4 mpaka tarahe 22 mwez Novemba.

Ikiwa huijui tarahe yako wenye majina yaliyoanza na herufi H na T wote ni watu wa Nyota ya Nge. Ikiwa unaijua tarahe yako angalia nyota inayoendana na tarahe yako hujui ndio uangalie jina.

   ASILI, SIKU, RANGI NA PETE ZA BAHAT

Asili ya nyota hii ni Maji, siku yao ya bahati ni Jumanne, namba yao ya bahati 9, Sayar yao ni Pluto. Malaika wa nyota hii Izraeel jini wao Abuu Muhriz al Hammar.

Rangi zao ni Urujuani nyekundu. Nge wanashauriwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi nzito yenye kutia shauku na kuvutia kama rangi ya damu ya mzee.

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi ya Kijani.Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Bluu.

Nge wanatakiwa wavae nguo zenye rangi inayong’ara, zenye kuonekana na maridadi, zilizo katika hali ya suti au mbili kwa pamoja. Nguo ziwe za rangi nyekundu au shati jekundu au skafu nyekundu. Kitambaa kiwe cha sufi au cha fulana au chenye kumeremeta. Mavazi yaendane na kofia na wanawake wapendelee sana kuvaa suruali

Vito vya pete zao ni Bloodstone, Malachite, Topaz. Ruby,Rhodochrosite, Kunzite, Moldavite, Opal, Diamond, Selenite, Quartz
Madini yao ni Chuma, Radiamu na Chuma cha pua na madini yao ni chuma.

Nge wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao, Mananasi, wapende sana vitunguu vibichi na vilivyopikwa, Nyama ya Kondoo mchanga na vyakula viambatane na viungo vikali.

Manukato yao ni ya Msandali,  mafusho yao  ni Qist. unachoma siku ya Jumanne kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

        NYOTA YA KUSHIRIKIANA NAYO

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Kaa na Samaki.Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Simba.Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Ndoo.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mshale.Nyota inayomsaidia katika Ubunifu ni nyota ya Samaki.Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Ng’ombe.

Nyota ya kutumia nayo au kustareheka nayo Kujifurahisha ni nyota ya Samaki. Kuwa makini kama utakuwa una mahusiano na mtu wa nyota hii mtakuwa mkitumia tu pasipo malengo ya maendeleo. Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Kaa na Mizani.

Hapa yatakiwa uwe makini katika kuanzisha mashirikiano ya kibiashara ama uhusiano au ndoa chunguza nyota na siku za kuanzisha hilo jambo lenu.

     TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Nge wana uwezo mkubwa wa uvuto au kuvutia watu katika mambo yao. Ni wenye uelewa mkubwa, majasiri katika kukabiliana na matatizo ambayo wengine yamewashinda.

Wana tabia ya kutilia mkazo mambo yao, tena kwa ukali na ikibidi kutumia ukatili ili jambo litimie wao wako tayari.Ni wasiri na wanaopenda kufanya mambo yao kwa siri sana. Kama ilivyo alama ya nyota yao hawaogopi kiza. Wana uwezo na kipaji cha asili cha kutekeleza mambo yao na wakafanikiwa.

Ni wenye akili nyingi, waerevu na wepesi sana kuelewa mambo. Nge vile vile wanaweza kujidhuru wao wenyewe mambo yanapowawia magumu. Wanapenda sana kutumia fursa ya kufanya mapenzi kama njia mojawapo ya kuonyesha ujasiri wao katika mapenzi na namna wanavyojua kufanya tendo la ndoa.
Kwao mapenzi au tendo la ndoa ni kiungo muhimu sana katika maisha yao hasa ikizingatiwa kwamba nyota ya Nge inatawala sehemu za siri.

Inashauriwa wale wenye moyo mdogo wasifanye mapenzi na Nge sivyo watajuta. Kitu kingine ni kwamba ni watu ambao hawayumbi na hawakubali kushindwa upesi.

Ni watu wenye ashki na hasira wakiwa wamedhalilishwa au wameumizwa na wapenzi wao na wanapofanya tendo la ndoa hasira zao huisha mara moja.

Ni watu wasiri sana katika masuala ya mapenzi na wanakuwa hivyo ili waweze kuwapata wapenzi wengi kukidhi matakwa au kiu yao kubwa ya ngono.

    VIPAJI, KAZI BIASHARA ZA NG'E

Kazi zinazowafaa wenye nyota hii ni kazi za madawa au tiba, kazi za upelelezi, kazi za utafiti, kazi za fundi bomba, kazi za elimu ya kale, na kazi za ushauri wa mambo ya mapenzi na ngono au biashara zinazoendana na mambo hayo.

Nge wana kipaji na uwezo wa kiroho wa kuwasiliana na watu katika kutekeleza mambo wanayohitaji. Mystical

Nge wanafanya kazi kwa kutilia mkazo na ushupavu wakihakikisha wanatekeleza malengo yao. Ni waerevu na wenye kung’amua mambo upesi. Ni wafanyakazi wazuri na wanaheshima kwa wafanyakazi wenzao.

            MAMBO YA KUZINGATIA

Nyota hii inatawaliwa na magonjwa ya  kifuko cha mkojo, uume, uke, kifandugu au kitonoko (coccy), mlango wa kizazi (cervix) na sehemu ya haja kubwa. Vile vile inatawala mfumo wa mkojo na tezi kibofu

Watu wa nyota hii wanatakiwa kujiepusha na tabia za Wivu, Kulipiza kisasi, Kutokubali Kusamehe, kutoshawishika au kutobadilika, kuwa mbishi, mng’ang’anizi.

Ikiwa nyota yako bado haijazungumziwa subiri makala zijazo soma makala zilizopita ambazo tayara zishafafanua nyota. Kichambuliwa private utalpia gharama

Una tatzo lolote la nyota, uzazi, nguvu za kiume, kukuza dhakar, mapenzi, biashara nk niachie ujumbe inbox

+255621442936

Whatsp group ni la malpo

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI