NYOTA NA TABIA ZAKE KATIKA MAISHA NA MAPENZI 'NYOTA YA MAPACHA'
HII ni makala ya tatu katika mfulizo wa makala 12 za nyota ambazo nimepanga kuzizungumzia hapa na leo tutazungumzia nyota ya mapacha. Tutagusia mafanikio siku za bahati namba za bahat na tabia zake katika mapenzi anayekuletea darasa hizi ni Mtabibi ASILI TZ.
Hii ni nyota ya tatu kwa uzawa katika nyota 12 watu wa nyota hii ni wale waliozalia kuanzia tarahe 21 Mei mpaka 20 Juni. Hapa namaanishia waliozaliwa kunazia tarahe 21,22,23,24 mpaka mwezi mei unapoishia na tarhe 1,2,3,4 mpaka kufikia tarahe 20 mwez juni wote nyota yao ni mapacha. Ikiwa hujui tarahe yako ya kuzaliwa kama una jina linaanzia heruf C,O,K na G pia nyota yao ni mapacha.
ASILI RANGI NA SIKU ZA BAHAT
Asili ya nyota hii ni Upepo, jinsia yake ni yakike sayar yake ni Uttwarid, siku ya bahat ni Jumatano namba ya bahat ni 6. Rangi za bahat ni bluu, njano na rangi ya chungwa. Rangi zinazowavutia kimapenz ni rangi ya samawati. Kifedha ni rangi ya fedha na kijivu.
Vito na pete za bahat kwa mwanaume upate pete ya chuma au fedha mwanamke dhahabu au fedha kito upate Agate, Aquamarine, Celestite au Quartz.Manukato ni marashi ya Mrujuani
Mafusho yao katika kutilia nguvu jambo lao ni Kashuu Muhlib kwa kiswahili kachiri. Yana asili na muonekano wa maua yana rangi ya kahawia. Kama utakuwa na jambo lako utachanganya na hayo mafusho utachoma siku ya jumatano kuanzia saa 12 mpaka saa 1 au kuanzia saa 7 mpaka nane
Kwa wanamitindo wanatakiwa kuvaa kisanii nguo nyepes suti na gloves, vitambaa vyao ni vya hariri
Malaika wake anaitwa Mikkail na jini wao ni Barkaan kama una bishara au mtoto mpe jina linalonziwa na T na siku ya kuanza biashara ni jumatano.
vyakula vinavyotawaliwa na nyota hii ni kuku, rasiberi, karoti na uduvi.
Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota hii wanashauriwa watembelee au waishi katika nchi au miji ifuatayo inayotawaliwa na nyota yao. Nchi hizo ni Ubelgiji na Wales, na baadhi ya miji ni London (Uingereza) na San Fransisco (Marekani).
NYOTA ZA USHIRIKIANO
Nyota za watu ambao anaoelewana nao ni nyota za Mizani na Ndoo. Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Mashuke, Mshale na Samaki. Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Samaki
Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Kaa, nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mizani. Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mizani. Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni Nyota za Ng’ombe na Ndoo.
TABIA HALISI KIMAUMBILE NA MAPENZI
Mapacha ni watu wenye hisia kali sana ambao wanakasirika upesi, ni watu wasiotulia na wenye uwezo mkubwa wa kujieleza na kuzungumza.
Wanaweza sana kushawishi watu. wanapenda sana mabadiliko na tofauti na kujua mambo, wanapenda watu na wanapenda kujumuika na watu lakini wakati mwingine hawaeleweki.
Wanapenda sana kusafiri na wanajulikana sana kwa hadhi yao ya kuwa na sura mbili. Kuna wakati wanakuwa na hisia tofauti na muda si muda wamebadilika. Pamoja na kwamba hawapendi kubanwa sana, ni watu wachamgamfu na wenye mahaba mazuri.
Katika Mapenzi wanahakikisha kwamba hawawachoshi wapenzi wao. Watatumia muda mrefu kuzungumza maneno mazuri na wapenzi wao ili kuhakikisha kuwa uhusiano unazidi kuwepo.
Katika mapenzi, wao wanapenda vitu au mambo tofauti tofauti, wakihisi wamechoshwa basi huwa wa kwanza kuondoka aidha kwa muda au moja kwa moja.Uaminifu ni kitu kigumu kwa Mapacha. Mara zote wanahisi kwamba kuna kitu wanakikosa nje hivyo basi wanatoka sana nje, hata kama wakiwa wana ndoa yenye furaha.Wengi wao wanafikia hatua ya kuishi maisha ya sehemu mbili; mke na bwana au bwana na mke.
Sifa zao ni kubadilika badilika katika mambo au maamuzi yao.Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni Kuwa na Fikra za ndani kuliko za juu juu.
Maadili yao ni Ujasiri katika mawasiliano, Uwezo wa kufikiria haraka haraka na uwezo wa kujua na kufahamu vitu haraka.
Tabia za kujiepusha nazo ni Kusengenya, Kuumiza wengine kwa maneno makali, Mambo ya juu juu na kutumia maneno ili kuwapotosha watu (Propaganda).
KIPAJI KAZI NA BIASHARA ZA MAPACHA
Weneye nyota hii wanatakiwa kufanya kazi za utangazaji Radio, Televishe, Matangazo. Uchapishaji wa vitabu ugungaji au uuzaji. Kazi za kufundisha au utoaji ushaur nasaha Uwakala wa kuwasafririsha watu nje ya nchi au utalii na ukalimani.
Wenye nyota hii wana kipaji kikubwa cha kuwasiliana na watu ambao wako mbali kwa kutumia akili zao au hisia walizokuwa nazo.
Wenye nyota hii hupenda kusumbuliwa na maradhi ya mikono, mabega, viganja na sehemu za juu za mbavu. Huweza kupata pumu, kifua, mafua kutokana na tatizo la kutopumzika kwa sababu ya kutafuta mambo mapya ndio yanayosababisha maradhi kwa wenye nyota hii.Wanasahau miili yao na mara nyingi wanapata matatizo ya neva kutokana na uchovu kwa mishughuliko mingi.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
Ufafanuzi huu unaweza ufuata kwa siku saa na rangi zake na kila ktu kilichoelezwa kulinganana na nyota yako. Kinachotafsr nyota ni tareh yako ya kuzaliwa ikia huijui tarhe yako ndo uangalie jina sasa kuna wengine mnajichana na maswali unaijua tareh yako alaf unaangalia na jina unakuta una nyota mbili tofaut fuata tarahe yako ndio halisi hujui tarehe ndo utumie jina.
Endelea kufuatilia makala zijazo kwa uvhambuzi wa nyota zinazoendelea, nimeshatafsiri nyota ya punda na ng'ombe. Ikiwa unahtja uchambuzi private utachangia gharama.
Una swali uliza hapa chini
Una tatzo lolote la afya uzazi, kazi, biashara, kesi kuibiwa kuuza, nguvu za kiume, uzazi, kukuza dhakar nk niachie ujumbe inbox
+255621442936
Whatsp group ni la malipo
Assalam alaikum, nimegunduwa watu wengi nyota zao haziendani na nyota za herufi zao mfano Mimi ni mezani lakini herufi ya mwanzo ya jina langu ni F hapa tuzingatie no I? "
ReplyDelete