UCHAMBUZI WA NYOTA PETE, SIKU ZA BAHATI MAFANIKIO NA MAPENZI 'NYOTA YA MIZANI'


HII ni makala ya saba katika zile nyota 12 ambazo nimepanga kuzizungumzia siku ya leo. Mashuke ni Nyota ya saba watu wa nyota hii ni wale waliozaliwa kuanzia tarahe 23 Septemba mpaka 22 Octoba. Ufafanuzi namaanisha wote waliizaliwa kuanzia tareh 22,23,24,25 nakuendelea mpaka mwisho wa mwez wa Septemba  na kuanzia tarehe 1,2,3,4 mpaka tarhe 22 octoba.


Km hujui tarahe yako ya kuzaliwa wale majina yao yalioanziwa na heruf G na S hawa pia ni nyota ya mizani. Kama unaijua tarahe yako ya kuzaliwa usishughulike na jiana fuata tarahe yako ikiwa huijui ndio ushughulike na jina. Nyota halisi ni tarahe yako ya uzawa.

     ASILI, RANGI, PETE NA SIKU ZA BAHAT

Asili ya nyota hii ni Upepo, Sayari yake ni Zuhura. Jinilsia yake ni dume hali yake ni thabiti uimaara. Jini wa nyota hii anaitwa Zawbat, malaika wa nyota hii Anyail. Siku yao ya bahati ni Ijumaa namba zao za bahati ni 6 na 9.

Manukato yao ni yenye asili ya uaridi, Rangi za bahati kwa wenye nyota hii ni Kijani isiyoiva. Blue pamoja na lavender rangi hizi huwafaa zaidi kwa sababu huwasilisha mapenzi,furaha na urafiki ambapo pia watu hawa hupenda sana kujihusisha na mapenzi na yanayohusu hayo.

Fusho la nyota hii ni ubani Mashatka kama una jambo lako basi dawa zako uchanganye na fusho hilo na ulichome siku ya Ijumaa kuanzia saa 12 mpaka saa moja asubuh au mchana saa 7.

Vito vya nyota hii kama ukipata pete za bahat basi iwekwe kito cha opal kwa ajili ya mafanikio kipesa au kipato na madini yake ni Copper.

watu wa nyota hii hufuatwa sana na Jini Mahaba sababu naye pia ni miongoni mwa majini wa nyota hii.

     USHIRIKIANO NA NYOTA NYENGINE

Watu wa nyota hii wanatakiwa washirikiane na Nyota ya Punda katika ndoa ama mapenzi. Nyota hiindio itakupa maendeleo na furaha katika ndoa. Nyota zinazoelewana nae kwa muda wote ni nyota ya Mapacha na Mshale.

Nyota ambazo haziendani ni ni Ng'ombe, Mashuke na Mbuzi. Nyota inayomsaidia kikazi ni Mapacha, msaada kipesa ni Mshale. Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni Mapacha. Nyota ya kutumia naye ni Punda

Nyota zinazomsaidia koushaur ya mambo ya kidini na kiimano ni Mshale na Samaki.

   TABIA HALISI KIMAUMBILE NA MAPENZI

Wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kupenda usuluhishi, amani na upatanishi. Ni watu wasikivu, watiifu, na wepesi kuongozwa. Ni wenye maumbo ya kupendeza hasa wanawake. Kwa ujumla ni watu wenye roho nzuri na wanajua kupenda na wenye mahaba mengi.

Ni watu wastaarabu, wenye adabu heshima na ni wakarimu kwa mtu yeyote na wanajipenda sana. Katika maisha yao wajipenda sana.

Kujihusisha na suala la mapenzi kwa wenye nyota hii ni kitu cha kawaida kabisa pamoja na kwamba wenye nyota hii wanachukua muda mrefu kufanya maamuzi na inawawia vigumu sana kuchagua kati ya wapenzi wawili yupi anaefaa. Kwao kuishi vizuri ni kuwa na mpenzi au uhusiano wa kimapenzi.

Watu wa mizani wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda sana kujionyesha kwamba wanapendwa.
Kwa sababu hizo wengi sana wanapumbazwa na mapenzi na ndoa zao zinakuwa zina
matatizo na zisizo na raha kwa sababu ya kuoa mapema bila kuangalia. Wenye nyota hii wanaonelea bora kuishi katika ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.

Katika suala la mahaba na ngono  wao ni mabingwa. Wanajua sana
kumpendeza mwanamke kwa maneno matamu yenye mpangilio na zawadi za thamani na wawapo kitandani wanatumia muda mrefu kuwachezea wapenzi wao sehemu nyeti.
Kwa ujumla wenye nyota ya Mizani wanapenda kuishi vizuri na wanapenda wapenzi wao nao waishi katika hali nzuri

Wenye nyota hii ni rahisi kupendeka na wenye ulaini wa mapenzi na ni watu wa kuvutia na wenye kuvutia kimaongezi kwa sababu wana kipaji cha kimvutia mtu kimaelezo na kumfanya ajihisi raha kuzungumza nao, wenye nyota hii ni watu wenye Tabasamu laini na wenye hisia za kimapenzi wakati mwingi na pia 

huonekana kama watu wa ajabu sana duniani,wao huzaliwa wakiwa na asili ya kujali wengine. Nyumba zao utakuta zimepambwa vizuri kwa maua kupendeza na mapambo ya thamani,nguo na manukato pia vinywaji huwa havikatiki ni nyota yenye kujipenda zaidi wao hufurahia kila kitu ambacho pesa inaweza kununua.

Nyota hii ni nyota ya mwenza hupenda sana kutembea na mtu na hawapendi kutembea peke yao hata barabarani 

Wenye nyota hii watu wakiwaangalia mara nyingi, huwaona kuwa ni watu wa muhimu sana hata katika familia au vikao vya ukoo mtu huyu huwa hasahauliki kwa sababu tu ya kuyatanua mawazo ya watu walioyatoa na lakini pia mara nyingine huonekana ni watu wanaoleta vurugu na ujuaji kwenye mijadala au wanakuwa ni watu wenye mitizamo tofauti na wengine na kuna muda huonekana wapumbavu kwa tabia yao ya kung'ang'ania kitu wanavyoelewa wao ndio na watu wengine waelewe hivyo hivyo kwa wengine muonekano wake wote huwaonyesha kuwa ni mtu asiye na maana kwa muonekano anaokuwa anajiweka hili huwa linamuumiza pia

ViPAJI KAZI BISHASHARA ZA MIZANI

Watu wa nyota hii kazi zao ni uhusiano wa jamii, Ushauri wa Ndoa, Biashara ya Sanaa, Ushauri wa Mambo ya Urembo, Uanasheria, Uhakimu pia biashara za kuziba pancha na kujaza upepo au kupamba maharusi zinawafaa zaidi
Kazini wenye nyota hii huwa ni washiriki wazuri na wenye upendo wa wafanyakazi wenzao na pia wenye nyota hii ni wajanja pia katika mbinu za kazi za ushirikiano nao huusishwa sana kwenye kazi za pamoja.

Wenye nyota hii wana kipaji cha kufumbua mafumbo na kujua siri za watu bila kuambiwa. na kuweza kumjua mtu vizuri kabla ya yeye kuanza kujielezea.
 
            MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
Wenye nyota hii hussumbuliwa sana na magonjwa ya mgongo hasa karibu na makalio ni watu wenye kusumbuka na figo pia na mgongo wa chini hasa kwenye maungio ya makalio na maambukizi ya figo huwa ni magonjwa yanapendelea sana nyota hii.

Ufafanuzi huu unahusiana na nyota yako siku na rangi za bahat kama una dawa unataka kufanya au biahsra mapenzi ndoa angalia siku nzur na muda wakufanya hilo jambo ikiwa ni mtu wa michezo ya kubahatisha angalia pia mambo muhimu niliyoyaorodhesha kwa kila nyota.

Ikiwa nyota yako bado haijzungumziwa subiri makala zijazo waliozaliwa kuanzia mwwz wa tatu tarehe 22 mpaka mwezi wa kumi tarahe 22 nyota zao tayar zishatolewa ufafanuzi angalia makala zilizopita ukihitaji uchambuzi private utalipia gharama.

Una tatizo lolote la kazi nyota, biashara, mapenzi, kuuza, kesi, kuibiwa nk niachie ujumbe inbox
+255621442936

Wahtsp group ni la malpo kwa whatja tu

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI