UCHAMBUZI WA NYOTA YA NDOO, SIKU, SAA RANGI, PETE ZA BAHAT, MAFANIKIO NA MAPENZI


AHLAN WASAHALA mpenzi mfuatiliaji wa darasa za ndoto nyota miti na mambo mengine yakidunia kwa madawa ya asili. Leo tunaendelea n uchambuzi wa nyota ya Ndoo anayekuletea darasa hizi ni Mtabibu ASILI TZ.


Hii ni nyota ya kumi na moja katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 20 Januari na Februari 18. Ufafanuzi ni wale waliozaliwq kuanziw tarahe 20,21,22,23,24 mpaka miwsho wa mwez Januar na kuanzia tarahe 1,2,3,4 mpakq tarahe 20 mwez February. Pia wale wenye majina  yalio anza na herufi K, W, H lakini hawa hawajui tarahe zao za kuzaliwa ikiwa unaijua tarehe yako fuata tarahe yako.

    ASILI, RANGI, SIKU NA PETE BAHAT
Asili yao ni Upepo.Malaika wake anaitwa  Kafyaeel, na Jini wao anaitwa Abuu Nuhu, Sayari yao ni Uranus. Siku yao ya bahati ni Jumamosi. Namba yao ya bahati ni 8

Rangi zao ni Bluu, Kijivu na Samawi ya Bluu. Wenye nyota ya Ndoo wanatakiwa wapake nyumba zao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi zilizotulia kama Bluu au Kijivu.

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Dhahabu na Machungwa. Madini ya Ndoo ni Uranium ikiwa ngumu kupata tumia risasi. Vito vyao vya kuvaa katika amethyst au Onyx 

Mafusho ya Ndoo ni Miatun- saila. unachoma siku ya Jumamosi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

Manukato yao ni yale yatokanayo na Mgadenia (Gardenia) na Azalea. Vyakula Matunda  ambavyo vinatawaliwa na nyota zao, vyakula vya nazi na nyama aina zote. Vile vile wapendelee kula Viazi Vitamu na Samaki Gamba.

                NYOTA YA KUSHIRIKIANA NAE

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Mapacha na Mizani. Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Nge. Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Ng’ombe.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Samaki.Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mapacha. Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Simba.Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mapacha.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Mizani na Mbuzi.

       TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Ndoo ni watu wachangamfu, wavumbuzi na wenye akili za kubuni jambo au kitu. Ni watu ambao wenye furaha wakati wote lakini inakuwa vigumu wakati mwingine kuwa karibu nao. Ni waaminifu na wakweli na wako tayari wakati wowote kutoa msaada unaohitajika.

Kwa upande mwingine ni watu ambao hawatabiriki hasa wanapokasirika, wanaweza kuwa wakaidi, wenye kushikilia jambo hata likiwa baya, ni wapotovu wa nidhamu na waasi.

Ni watu ambao hawajali Dunia inasema nini au inafikiria nini, wakati mwingine hukataa shughuli za kijamii na kujihusisha katika mambo yasiyo na maana yeyote.
Kwa ujumla ni watu wenye Roho nzuri ya kibinaadamu wanapenda kutoa msaada pamoja na kwamba wakati mwingine wanakuwa siyo dhahiri.

Ndoo ni watu wanaopenda uhuru na hawawezi kabisa kukubali kudhibitwa katika mapenzi, mawazo yao na miono yao inaweza kubadilika mara moja na kuwa wakaidi na wasumbufu. Pamoja na kwamba ni waaminifu na wanatoa msaada mkubwa kwa wapenzi wao.

Wako tayari kutulia katika mapenzi iwapo watahakikishiwa uhuru wao na haki ya kutoingiliwa katika mambo binafsi. Ni watu ambao hawapendi kuonyesha hisia zao halisi na wanachukua muda mrefu kuingia kikamilifu katika uhusiano wa kimapenzi.

Mara nyingi inakuwa vigumu kwao kuwaamini wapenzi wao lakini wakisha waamini wanakuwa waaminifu.
Ni watu ambao husema mambo bila kuficha na mara nyingi hawaeleweki kwa wapenzi wao.

Katika ngono, kwa sababu ya kupenda uhuru huwa wanapenda kufanya mambo wanavyotaka wao na hawakubali kuingiliwa.
Wakati mwingine hushindwa kuelewa hisia za wapenzi wao jambo ambalo linawafanya wapenzi wao washindwe kuwaelewa.

Matakwa yao ni Kujua na Kuleta mambo mapya.
Tabia za kujiepusha nazo ni Kutojali, kutoshawishika au kutobadilika, kuwa na mawazo yasiyobadilika.

           VIPAJI KAZI BIASHARA ZA NDOO

Watu wa Ndoo ni wenye mawazo ya ubunifu na wenye kugundua njia mpya na zenye uhakika katika kazi.
Kazi zinazowafaa ni za uhandisi wa umeme, kompyuta, utafiti wa Sayansi, utabiri, huduma za jamii na utafiti wa mambo ya kale.

Ndoo wana kipaji cha kutoa tafsiri sahihi ya jambo lolote linalotokea wakati wowote, Sudden Revelation.

Kazi zao wanazifanya kwa upole na uhakika, pamoja na kwamba wanafanya kazi kwa bidii mara nyingi huwa wanaonekana hawajafanya kitu au sifa huenda kwa watu wengine.

Kwa uhakika mawazo yao saa zote yanafanya kazi. Ni watu ambao muda wote wanafikiri njia mpya na za uhakika za kutekeleza wajibu wao na kikazi.

    MAMBO MUHIMU YAKUZINGATIA

Nyota hii inatawala kifundo na ugoko. Wenye nyota hii wana mawazo mapana ya kufanya mabadiliko ya Dunia na hii inawasababisha wajisahau hasa katika afya zao na mara kwa mara hupata matatizo ya kuugua.

Kutokana na ubishi wao mara nyingi wanakuwa wabishi kupokea ushauri kuhusiana na hali zao za kiafya.
Matatizo yao makubwa yanasababishwa na kuchoka kwa misuli kutokana na kazi nyingi, kwa kawaida ni wagonjwa wabishi wasiopenda ushauri.

Wanapofanya mazoezi wanashaurwa wasiwe na hasira kwani hiyo inawafanya wajiumize au wapate ajali ndogo ndogo hasa sehemu za miguu, ugoko, vifundo na uvimbe katika sehemu hizo.
Vile vile matatizo yao mengine ya kiafya ni mzunguko wa damu na mishipa ya miguu.

nyota yako inaongozwa na tarahe yako ya kuzaliwa ikiwa huijui ndio uangalie herufi. Kama unaijua angalia tarahe yako.

IKIWA NYOTA YAKO HUJAIONA BADO ANGALIA MAKALA ZILIZOPITA TUSHAFAFANUA NYOTA ZOTE IMEBEKI MOJA TU YA SAMAKI, UKIHITAJI UCHAMBUZI BINAFSI UTALIPIA GHARAMA.

una tatzo lolote kazi, nyota, biashara, mapenzi, kesi, kuibiwa, uzazi, nguvu za kiume, kukuza dhakar nk niachie ujumbe inbox

+255621442936

Whtso group ni la malipo
www.tabibuasili.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI