UCHAMBUZI WA NYOTA, RANGI, SIKU, PETE ZA BAHAT, MAFANIKIO NA MAPENZI 'NYOTA YA MSHALE'


HUU ni mfululizo wa cuambuzi za nyota kuhusiana na siku rangi za bahati ushirikiano katulika biashara na mapenzi pamoja na pete za bahati. Leo tunazungumzia nyota ya mshale ikiwa ni nyota ya tisa katika idadi ya nyota 12 za uzawa. Anayeekuletea darasa hizi ni Mtabibu ASILI TZ.


Watu wa nyota hii ni wale waliozaliwa Novemba 23 mpaka 20 Disemba. Ufafanuzi ni wote waluozaliwa kuanzia tarhe 23,24,25 mpaka mwisho wa mwez Novemba na kuanzia tarahe 1,2,3,4 mpaka tarahe 20 mwezi Disemba. Wale wasiojua tarahe zao za kuzaliwa basi wale wenye majina yanayoanziwa na heruf I na U

    ASILI, SIKU, RANGI NA VITO VYA BAHATI

Asili yao ni moto, jinsia yake ni dume Siku yao ya Bahati ni Alkhamisi. Siku mbaya ni Jumatatu na Jumanne Namba yao ya Bahati ni 5 au 7, Sayari yao ni Mushtara.

Malaika wake anaitwa  Israfeel na Jini anayetawala alkhamisi anaitwa Shamhuurush Kadhi . Rangi zao ni Bluu na Bluu iliyokolea. 

Wenye nyota hii wanatakiwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara rangi zenye kusisimua na uchangamfu na zinazoashiria hali ya kumkaribisha mgeni. Rangi hizo ni Nyekundu iliyochangamka rangi ya Zambarau  na rangi ya hudhurungi au kahawia.

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Njano na Njano-machungwa.Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Nyeusi na Bluu iliyoiva. Hapa ufafanuzi utatumia rangi ya bahat ya nyota yako kulingana na tukio husika unalotaka kulifanya.

Madini yao ni bati na pete zao ziwe za bati au fedha  Manukato yao ni Yasmini.  Vito vyao vya kuvaa katika pete ni Yakuti ya njano au Lapis LazuliMafusho ya Mshale ni Udi Kafur. unachoma siku ya Alkhamisi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

Vyakula na matunda ambayo vnatawaliwa na nyota yao. Nyama mwitu, kunazi za rangi ya bluu, maboga na juice ya mapera. Mshale wanatakiwa wavae nguo zenye kuathiri na za mzaha mzaha kama koti au blauzi isiyo rasmi au nguo za kitamaduni zilizoongezwa ongezwa vitu vingi kama maua au nakshi nakshi. 

      NYOTA YA KUSHIRIKIANA NAYO

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Punda na Simba. Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mashuke.Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Samaki.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mbuzi.Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Punda.Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Mapacha. Ikiwa unataka kupunwa au kujifurahisha ni nyota ya Punda.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Simba na Nge.

     TABIA ZAO HALISI KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:

Mshale ni wenye tabia ya kuwa na matumaini ya mafanikio kwa lolote wanalolitegemea. Wanapenda kuwa na uhuru wa kupenda na kuchagua na wanapenda watu wengine wawe kama wao.
Hawapendi mambo nusunusu. Ni watu ambao wako wazi na wanaopenda kusoma. Ni wakweli na ukitaka kuelewana nao na wewe uwe mkweli.

Mshale ni watulivu, waaminifu na wanapenda uadilifu,.hawapendi kuamrishwa kufanya jambo kwa sababu wanaamini kwamba wao wenyewe wana uwezo mkubwa wa kutekeleza jambo lolote, lakini likiwaudhi wanakuwa wakaidi na wasioweza kutii amri.
Wenye nyota hii hawaoni taabu kusema lolote bila kujali athari zake, mradi jambo hilo liwe la kweli.

Pamoja na kwamba wenye nyota hii wanapenda wawe huru na wenye kujiamulia mambo yao wenyewe, huwa wana starehe na kuona raha wanapokuwa ndani ya uhusiano wa kimapenzi.wanapenda sana kujihusisha na makundi makundi lakini huwa wanapata muda wa kuwa na wapenzi wao. Katika mapenzi ni wachangamfu na wenye kupenda lakini tabia yao ya kutojali inawafanya wapenzi wao wajione kwamba wanakosa ulinzi wa kimapenzi.

Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu. Mwanzoni wanakuwa wagumu sana kujihusisha. Wanapenda sana wakati wote kuwa na wapenzi wapya au mapenzi ya kawaida kwa sababu wanaamini mapenzi ya kudumu yanawanyima uhuru.
Wapenzi wao wanaponyesha dalili ya kuwapenda basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu ya kubanwa na kutokuwa na uhuru.

Ni watu wanaopenda kufanya ngono kwa muda mrefu na hisia zao ziko mbali, inashauriwa kwamba wapenzi wao wawe wamekula kabla ya tendo la ndoa vinginevyo itakuwa taabu.

Maadili yao ni Ukweli, Kuona mbali, Ukarimu na Kuwa na uwezo wa kusikiliza mawazo ya wenzake japokuwa siyo lazima akubaliane nayo.

     VIPAJI KAZI BIASHARA ZA NYOTA HII

Mshale ni waaminifu wanaopenda sana mafanikio, wako tayari wakati wowote katika kazi. Kutokana na hili wana bahati ya kuwa katika sehemu muafaka na katika muda unaotakiwa.

Wenye nyota hii ni wafanyakazi waaminifu na hawapendi kuwasimamia watu katika kazi. Wanawaamini wafanyakazi wao na wanapokuwa ofisini huleta mazingira ya urafiki na kuaminiana.
Kazi zinazowafaa ni za usafiri, kazi za sheria, Wakili au Hakimu, kazi za uandishi, ualimu, dini, sheikh au padri au makanisani au misikitini, michezo, kazi za kijeshi na uuzaji.

Mshale wana kipaji cha kutabiri na kujua mambo ambayo yatatokea mbele au muda utakaokuja, na mara nyingi wanalolisema huwa linatokea hata likiwa la kipuuzi.

          MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA

Tabia za kujiepusha nazo ni Kutegemea mambo kuwa yatakuwa mazuri siku zote, Kutia chumvi mambo na Kuzidisha Ukarimu kwa kutegemea hela za watu wengine.

Magonjwa ya nyota hii ni maumivu chini ya kiuno. Wenye nyota hii hawapendi kuugua. Lakini huwa wanapata maradhi kutokana na kujishughulisha kupita kiasi na kutumia nguvu zao na akili zao kwa muda mrefu bila mapumziko. Wanathamini sana mizunguko kuliko mapumziko.Vile vile ni watu wasiopenda ushauri kuhusiana na afya zao. Wanashambuliwa sana na majereha na maradhi ya nyonga, mapaja, maradhi ya ini  kupooza kwa miguu na ugonjwa wa kuumwa mishipa au misuli ya nyuma ya paja.

Tatizo lao lingine ni kuwa wanapenda sana kula na kunywa na hiyo huwaletea unene usiotakiwa. Wakitaka kujikomboa na matatizo wanashauriwa wawe na tabia ya kujipumzisha.

Tumebakisha nyota tatu ikiw hujaona nyota yako fuatilia makala zilizopita kwenye ukurasa wangu. Uchambuzi private utachangia gharama

Una tatzo lolote la afya, uzazi, nguvu za kiume, kukuza dhakar, nyota, biashara mapenI, kesi uzazi nk niachie ujumbe inbox

+255621442936

Whatsp group ni la malipo

Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI