NYOTA SIKU, NAMBA, RANGI ZA BAHATI MAFANIKIO NA MAPENI 'NYOTA YA SIMBA'
UHALI gani mpenzi mfuatiliaji wa darasa zangu zinazohusiana na maradhi mbalimbali, uchambuzi wa nyota na mambo mengine yakidunia. Leo tunaendelea na uchambuzi wa nyota katika mafanikio ya kimaisha na mapenzi na leo tunazungumzia nyota ya Simba anayekuletea darassa hizi ni Mtabibu ASILI TZ. unaweza pata darasa hizi kupitia page yangu hii au group la dawa za kisunna na tiba asili hapa facebook au group la whatsap kwa kulipia.
Nyota ya Simba ni nyota ya tano katika zile nyota 12 na watu wa nyota hii ni wale waliozaliwa kuanzia tarehe 23 Julai hadi tarahe 22 Agosti. Ufafanuzi wake ni wale wote waliozaliwa kuanzia tarehe 23,24,25,26 mpaka mwisho wa mwez Julai na wale waliozaliwa kuanzia tarahe 1,2,3,4,5 nakuendelea mpaka tarahe 22 Mwez Agost hawa wote nyota yao ni Simba.
Na wale ambao hawazijui tarehe zao za kuzaliwa basi kama jina lako linaanzia na heruf E,Q,S n T wote hao nyota yao ni Simba. Ikiwa unaijua tarhe yako ya kuzaliwa achana na na kufuatilia jina lako maana nyota halisi ni tarhe yako ya kuzaliwa.
ASILI, RANGI, SIKU NA NAMBA ZA BAHAT.
Asili ya nyota hii ni Moto jinsia yake ni ya kiume, Malaika wake ni Raukayeel jini wao anaitwa Abdullah Saeed al Madhhabsayar yake ni Jua, siku yake ya bahati ni Jumapili namba zake za bahati ni 1,3,4,10 na 19.
Rangi zao za bahat ni nyekundu, dhahabu na rangi ya machungwa. Ndio maana hata timu ya Simba huzaa rangi nyekundu na ikiwa inacheza siku ya Jumapili ushindi upo wazi kwa asilimia kubwa.
Madini ya Simba dhahabu kama pete itapendeza ikiwa ya dhahabu vito vyake ni Ruby na Peridot. Mafusho yao ni Sandarus yachomwe siku ya Jumapili kuanzia saa 12 mpaka saa moja asubuh au kati ya saa saba mpaka saa nane mchana.
Vyakula na matunda nyota hii ni nyama nyekundu kama ng'ombe, mbuzi, kondoo, maboga, machungwa, ndimu na limao.
Ukipata fursa yakutembea nchi zao ni Italia, Morocco na India. Mavazi yanayowapendeza yawe ya kifalme kitajiri au machifu, vitambaa vyao ni vya hariri au valvet kulingana na rangi nilizozitaja hapo juu kama utaweka mapambo ya dhahabu itakupa nguvu na bahat zaid. Kwa wanwake wapate magaun maref ya rang ya dhahabu nyekundu au chungwa aina ya vitambaa n hvyo nilivyovitaja.
NYOTA YA KUSHIRIKIANA NAE
Nyota zinazoelewana na nyota hii ni Punda na Mshale. Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Ng'ombe, Msaada wakipesa ni Mashuke, msaada katika ubunifu ni nyota ya Mshale. Nyota ya kimapenzi na ndoa ushirikiano wa kifedha ni nyota ya Ndoo. Ukitaka kutumia kutanua mtu wa kukulia fedha ni Mshale. Ukihitaji msaada wa kidini au imani ni Punga na Kaa.
Nimefafanua nyota za kusirikiana nazo kila pahala na nyota ya kuoa, ila kuna nyota ukianzisha nayo mahusiano au bishara wewe ndio utatoa zaid kwa lugha nyepes utakuwa unahonga sana atahitaj kila kitu na hutapinga kulingana na uzito wa nyota yake kwako.
TABIA HALISI ZA KIMAUMBILE
Wenye nyota hii huwa ni wabunifu, wanashauku, wakarimu, wanamoyo, wanapenda usafi furaha kutabassamu. Ila wamejawa na kiburi ukaidi wanapenda kujitegemea, wqna uvivu kwa kiasi fulan, pia huwa wanajitoa ufahamu. Wanachukia sana ikiwa utawapuuza maana wanapenda waonekane wao wafalme au malkia hata katika kuchangia kitu wanataka wao ndio waanze wengine wafuate nyuma yao
wanapenda ufahari mkubwa na kutukuzwa. Wanapenda kutumia na wanataka waonekane kwamba wana hali nzuri, wanapenda sana kuheshimiwa.
watu hawa huwa ni wakali sana katika mapenzi na mara nyingi huwa hawadumu kwenye mapenzi kutokana na ukali wao na huwa ni watu wenye ghadhabu za mara kwa mara hasa akikosewa au akipingwa kidogo tu, kimapenzi
Jambo kubwa walilonalo ni uwezo wa kuvumbua mambo ambayo watu wengine hawajui.
Ni watu wakarimu lakini wajeuri na wanapenda sana kuonea watu. Wana hisia kali, ni wakali na wanakiburi.Tabia yao ni kujitanua, Ukarimu na ulezi ikichanganyika na ujeuri na kujionyesha, huwaharibu wale wanaowapenda.
Furaha haina mpaka katika mapenzi ya Simba, mioyo yao mikubwa na hisia zao nzito hutokeza dhahiri wanapompenda mtu. Baada ya hapo ndipo sura kamili ya Simba hujitokeza.
Wao wanathamini sana mapenzi na juu ya jambo lolote, na wanaweza kuwa waaminifu sana na wakati mwingine huwaabudu wapenzi wao.Wanapenda kujishughulisha sana na mambao ya mapenzi lakini mambo yakiharibika inakua vigumu sana kuyatengeneza.
Tatizo lao kubwa ni kujisahau Kwa nje wanaonekana ni wenye kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani wanaweza kuwa wanaumia lakini hawawezi ksema mbele za watu juu ya hisia zao.
Wanauwezo mkunwa wa kuzalisha au kubuni vitu vya kuzalisha fedha lakini fedha zao huwa hazikai. Wana bahati sana hasa kulingana na nyota yao, katika maswala ya kiuchumi, japo kuwa ni nyota ya watu wenye kutumia sana pesa hovyo na inayeyuka kama vile moto vile vile watu wenye nyota hii ni watu wenye kuogopwa sana na kukimbiwa na watu kutokana na ukali wao.
mara nyingi huwa na marafiki wengi kutokana na kuwa na ukarimu na uaminifu, hii ni kama vile jua linavyounganisha sayari nyingi na kuwa source ya nishati,
na hisia zao za ucheshi ndio huwafanya kuwa karibu zaidi na watu wengi sana.
VIPAJI KAZI NA BISHARA ZA SIMBA
Watu wa Simba wanatakiwa wafanye kazi za Usimamizi katika sekta binafsi au Serikalini au makampuni ya biashara. Uongozi katika sekta ya michezo.
Kazi za kujiajiri ni michezo, usonara, kutengenrza au kuuza mavazi, Mwanamitindo, Uigizaji, Ualimu, pia wanauwezo wa kuvumbua au kuanzisha jambo likawa kubwa na wengine wakawaiga.
Nyota hii hukumbwa sana na maradhi ya moyo, sehemu ya juu ya mgongo na bandama, maumivu katika uti wa mgongo. Pia hupata shinikizo la damu la juu na chini na maradhi ya moyo na homa za Uti haziendagi mbali.
Endelea kufutilia makala zijazo ikiwa nyota yako bado haijagusiwa, endelea kifuatilia makala zijazo nyota zilizopita soma makala za nyuma
Una tatzo lolote la uzazi nyota biashara mapenz kesi kuibiwa kuuza nk niachie
+255621442936
Whtsp group ni la malpo
Asante. Sana kwakuniwezesha kujuwa nyota yangu
ReplyDelete