UCHAMBUZI WA NYOTA YA SAMAKI, RANGI, SIKU, PETE ZA BAHATI, MAFANIKO NA MAPENZI
HII ni makala ya mwisho katika mfululizo wa makala 12 ambazo niliziahidi kutolea ufafanuzi wa nyota. Ufafanuzi ambao ulihusiana na rangi za bahati siku pete za bahati mafanikio katika biashara mali na mapeniz. Na hii ndio makala ya mwisho ya uchambuzi na leo nazungumzia nyota ya Samaki, makala hizi zinaandaliwa na Mtabibu ASILI TZ.
Ikiwa umepitwa na hizo makala kumi na moja soma post zilizopita kupitia ukurasa wangu ili ujue nyota yako na uchambuzi wake kwa kina. Ukihitaji uchambuzi binafsi utachangia gharama za uchambuzi hii namaanisha wale wanaotaka kuchambuliwa inbox hivi vtu kwa kina itakupasa utoe ujira.
Samaki ni nyota ya 12 katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 19 Februari na Machi 20. Ufafanuzi ni watu waliozaliwa kuanzia tarahe 19, 20,21,22,23 mpaka mwisho wa mwezi Februar na kuanzia tarahe 1,2,3,4 mpaka tarahe 20 mwezi March. Wale wasiojua tarehe zao ni watu au wenye majina yalio anza na herufi L na X na wote ni Nyota ya Samaki.
ASILI, RANGI, SIKU NA PETE ZA BAHATI
Asili yao ni Maji. Malaika wake anaitwa Israfeel, jini wakeaanaitwa Shamhuurush huyu ni Kadhi au kiomgozi wa Majini. Sayari yao ni Neptune.Siku yao ya Bahati ni Alhamisi, Namba yao ya Bahati ni 8.
Rangi zao ni Bluu iliyochanganyika na Kijani na Aqua. Rangi zinazowapa uwezo wa Mapenzi, Mahaba na Furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Udongo, Njano na Njano-machungwa.
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Nyekundu. Wenye nyota ya Samaki wanatakiwa wapake nyumba zao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi ambayo haijakoza ya Bluu au Kijani au Urujuani.
Madini ya Samaki ni Platnum ikiwa ngumu kupata tumia Bati Kwa ajili ya pete. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni Aquamarine au almas nyeupe
Mafusho ya Samaki ni Udi Kafur. unachoma siku ya Alkhamisi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.Manukato yao ni Yungiyungi.
Samaki wanashauriwa wapende kula matunda au vyakula vifuatavyo. Matunda ya Kunazi, Nyama mwitu kama Swala, Nyati na kadhalika.Vile vile wapendelee kula Maboga.
MASHIRIKIANO YA KINYOTA
Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Kaa na Nge.Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mshale.
Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Mapacha. Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Punda.
Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Kaa.
Nyota nzuri na bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano katika biashara ni nyota ya Mashuke.Nyota ya kujifurahisha ni nyota ya Kaa.
Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Nge na Ndoo.
TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Watu wenye nyota ya Samaki ni wenye huruma, wapole na wenye moyo mzuri, hawawezi kukubali kumuona binaadamu mwingine akipata taabu au uchungu. Kwa hakika ni watu ambao wana hisia kali kwa wengine, hawajipendelei na wako tayari wakati wowote kujitoa mhanga ili watu wanufaike, mapenzi yao au huruma kwa binaadamu wengine hayana masharti yeyote.
Nafsi zao zimegawanyika katika nafsi ndogo ndogo kama vile muathiriwa mwenye kujitoa mhanga, mwokozi, na mkombozi.
Hayo yote yaliyotajwa wanaweza kuyatekeleza inapohitajiwa na akishatumbukia katika moja ya mambo hayo huwezi kumtoa.
Kwa ujumla nafsi za Samaki siyo za kidunia, ni watu wabunifu na wenye ndoto za kufikiri mambo ya baadaye na katika maisha yao, wanaona raha sana kuwa na mawazo ambayo yatawaepusha na ugumu wa maisha.
Ikiwa wamekwama katika jambo lolote basi wataitafuta faraja au watajituliza kwa ulimwengu wao wa mawazo. Samaki ni wenye kukamilika na Mahaba mengi na wanapenda sana kujitumbukiza na kuzama kwenye dimbwi la mapenzi.
Kuwa katika mapenzi ni kitu wanachokipenda na kukifurahia sana. Ni waangalifu wazuri kwa wapenzi wao wana huruma nyingi.
Wana hisia kali za kimapenzi na ni wepesi kuathirika.
Mara nyingi huwa waoga wa vitu vya kimapenzi kwa sababu ya kuogopa kuvurugika kwa mipango yao ya baadaye.
Samaki huyachukulia mapenzi kama ua la waridi na wanawaona wapenzi wao kama binaadamu wasio wa kawaida.
Tatizo lao kubwa la kimapenzi ni kwamba wanawaamini sana wapenzi wao na wanakuwa na mawazo au firika za kimapenzi ambazo hazipo katika dunia hii.
Kwa ujumla wenye nyota hii wanapokuwa katika mapenzi wanakuwa wamejawa na shauku na mifano ya kuvutia na wanapenda wapenzi wao waishi kiroho. Mategemeo yao yanakuwa makubwa na yasipotimia huwa wanavunjika moyo.
Maadili yao ni Uvumilivu, Utiifu, Ustaamilivu, Kuratibu, Kuandaa na Uwezo wa kuona mbali. Matakwa yao ni Kutawala, Kusimamia na Kuongoza. Tabia za kujiepusha nazo ni Kutokutegemea kuwa mambo mabaya yatatokea, Kuwa na masikitiko, Kutokupenda mabadiliko na Kupenda vitu na mali kupita kiasi.
KIPAJI KAZI NA BIASHARA ZA SAMAKI:
Kugundua muelekeo wa kimaisha kwa Samaki wakati mwingine huwa ni matatizo.
Tabia yao ya kushughulikia sana binaadamu wengine huwafanya wasiwe na muelekeo.
Wanatakiwa wafanye kazi ambazo zinazohusiana na kusaidia watu. Kipaji cha kutafsiri mambo, huwasaidia vile vile kufanya kazi za sanaa kama vile kupiga picha na kazi za muziki au maigizo.
Kazi zingine zinazowafaa ni za kuhudumia wagonjwa, kucheza shoo, uaskari wa majini kazi za dini au kazi za kutoa ushauri nasaha.
Samaki wana wana kipaji cha kufikiria jambo na kuliunda na likawa vile walivyotaka wao
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
Nyota hii inatawala nyayo na vidole vya miguu. Matatizo yao ya kiafya yanakuja pale wanaposhindwa kutekeleza ndoto zao au mipangilio yao kimaisha au wanapokorofishana na wapenzi wao.
Wanapoathirika na hayo yaliyotajwa hukimbilia kwenye ulevi na utumiaji vidonge uliokithiri.
Tatizo lingine ni maradhi ya nyayo za miguu, uvimbe unaotokana na baridi kali hasa katika vidole vya miguu.
Hii ni makala ya mwisho ya uchambuzi wa nyota soma makala zilizpita kupitia ukurasa wangu ili kujua nyota yako. Uchambuzi private utagharami. Mambo muhimu zingatia tarhe yako ya kuzaliwa angalia siku z bahat ikiwa unataka kufanya jambo anzia siku hiyo yenye bahay na nyota yako. Ikiwa unafanya dawa basi changanya na hayo mafusho ya nyota yako ili upate majibu haraka.
Una tatzo lolote la uzazi, nguvu za kiume, kukuza dhakar, biashara, mapenzi, kazi, ndoa, kuuza nk kwa mafanyo na dawa niachie ujumbe inbox
+255621442936
Whtsp group n la kulpia
Comments
Post a Comment