KUWAONA WAZEE 'AJUZA' 'NYANYA' NDOTONI WALIOKUFA NA WALIO HAI NINI MAANA NA TAFSIRI YAKE




  LEO tutazungumza kuhusiana na ndoto zinazowahusu vikongwe ajuza. Ikiwa unaota alaf kwenye ndoto yako kuna taswira ya mzee ni nini maana yake na nini unatakiwa kukifanya hii ndio anuani ya somo letu la leo fuatana nami mpaka mwisho wa makala haya ili kufaham zaid.


   Ndoto hizi zimegawanyika katika sehemu mbili, moja kuna kuota wazee waliokufa bimaana watu ambao unajuana nao. Pili kuna kuota kuona wazee ambao huwajui kabisa na hujawahi kukutana nao. Kwenye ndoto za wazee waliokufa hapa nitazungumza na watu wako waliokufa ambao unawaota ndotoni.

         KUWAONA WAZEE WALIOKUFA
  Ukiota mzee aliyekufa anakuomba kitu au msaada ni ishara ya kuwa alipo anahitaji dua na maombi kutoka kwenu ninyi mliopo hai. Hapa pia ukiota mtu aliyekufa yupo katika hali mbaya au anakuhadithia kitu cha kusikitisha juu yake, ninaposema hali mbaya siwez kuorodhesha mambo yote ila namaanisha akiwa katika hali ya hudhun mfano kaaachwa na usafr kanyimwa chakula anachapwa anaumwa yupo dhaifu yapaswa ufanyie visomo.

  Ikiwa utamuota akiwa kwenye furaha ni ishara kuwa alipo yupo sehem nzur lakn pia whtajika uzidishe dua kwake ili awe salama zaid. Kama utakuwa unawaota sana watu waliokufa wazee ikiwa watu hao walikuwa watu wema bimaana wacha mungu kuna ishara mbili moja kifo chako kipo karbu lakn pili unatakiwa kuish maisha walioish wao ikiwa uliowaota ni masheikh basi kuna karama ya usheikh utaipata ikiwa walikuwa ni matabibu basi nawewe utatibia siku za usoni.

  Ikiwa wazee uliowaota mara kwa mara walikuwa ni wachawi washirikina basi pia tafsr ya kwanza kifo chako kipo karbu pili utafanya shughuli walizokuwa wanazifanya wao ikiwa ni uchawi au mambo ya matambiko ikiwa wataka kujitoa ni kujiwahi mapema kwa matibabu. Ikiwa unaota mzee bibi au babu anakupa kitu akiwa katika mavazi meusi ikiwa anakulazimisha ni ishara ya mambo ya kimila yenu watakiwa uyarithi ikiwa ni uchawi matambiko nk.  

    Ikiwa utamuota mzee babu anakupa kitabu na amevalia mavaz nadhifu utarithi kazi yake aliyekuwa akiifanya km ni sheikh imamu padri mtabibu kwa maana mganga basi ujiandae na hizo shughuli. Ikiwa utawaota wazee waliokufa wapo kikaon na wewe upo na umewekwa kama mgen rasm ni ihsra ya kurithishwa uchawi kuwa kiongozi wa matambiko nk.

   KUWAONA WAZEE WALIO HAI NA USIOWAJUA
 

  Hapa tunazungumza wazee walio hai na wengien huwajui sasa aweza akawa hai au amekufa lakini wewe hujawahi onana nae hata siku moja.

   Ukiota unamuona mkweo ndotoni utaugua, ukiota unamuona mama yako mzazi akiwa katika furaha utafanikiwa katika mambo yako na akiwa katika hali ya kukasirika mambo yako yataenda kombo. Ikiwa utamuona mzazi wako ukamuita akaondoka au kakuona akakupita jua ana kinyongo kuna jambo umelifanya hajalipenda fika kwake muombe msamaha kabla hajafa.

    Ikiwa uliyemuota mzazi wako amekufa na umeota anakupita au umemsemesha hajibu yupo katika sura yakukasirika inashiria katika maisha ya kawaida kabla hajafa uliwah kumuudh na umechelewa kumuomba msamaha au kuna jambo alikukataza wakat wa uhai wake na wewe unalifanya.

  Ukiota upo na wazee wa mtaani kwako au kijiji kwenu kila mara na ukiamka asubuhi lazima ukutane nao na huwa wanakuchangamkia hapo kinachotafsiriwa ni matendo ya ndoto ikiwa ni vikao vya maporini sherehen ishara ya kuingizwa kwenye chama cha uchawi ikiwa unafanyisha kazi tu na ukiamka umechoka ni ishara ya kufanyishwa kazi usiku

Kuonana na ajuza aliyejipamba ni ishara ya mambo yako yatanyooka ahad zitatimia kama kuna kitu unauza kitatoka haraka. Ukimuona mzee ndotoni ana sura mbaya ya kutisha mambo yako yataenda kombo kama una ahad pahala haitatimia kwa wakati au isitimie kabisa. Ukiota ajuza yupo uchi ni ishara ya kufedheheka kuna kitu kitakushushia heshima yako.

Ukiota ajuza wanakula nyama ni ishara ya kusengenywa au hata watu wa kawaida ukiwaota wanakula nyama ishara ni hyo ila ukiwaona wamezd idadi na wapo porini wanakula nyama na wewe ukiwepo ni ishara ya kuingizwa kwenye vyama vya wanga pia wewe mwenyewe ukiota unakula nyama ina maana mbili moja utasengenya pili ni ishara ya wanga ikiwa unaota sana nyama mara sherehe ni ishara ya chama cha uchawi.

Ukiota ajuza ana maziwa makubwa ishara ya mafanikio na utapata unachokihitaji

 Kikubwa ni kuzingatia kile unachoota na kukifanyia ufumbuzi, ikiwa huoti kabisa ukiota unasahau ni ishara ya vifungo.
 Maswali kuhsu ndoto yaulizwe hapa chini inbox utachangia

Una tatzo la afya uzazi nguvu za kiume biashara mapenz kuibiwa kesi nk niachie ujumbe inbox

+255621442936 
Whatsp group ni la kulpia kwa wanaohtaj

Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI