UKIOTA UMEKUFA UKIOTA UNAONA MAITI NDOTO ZA VIFO NA MAZINGIRA YAKE ISHARA NA TAFSIRI



Kama nilivyozungumza katika makala ya awali kifo ni mwisho wa mwanadamu na ni mwanzo wa maiti. Kwa hiyo ukiota kifo inaashiria ni mwisho wa jambo fulani na ni mwqnzo wa jambo jingine yweza ikawa kutoka kwenye ubaya kwenda kwenye wema au wema kwenda ubaya huzuni kwenda furaha umasiki kwenda utajiri na kinyume chake


UKIOTA UMEKUFA NA KUFUFUKA

Utafanya madhambi na utamuomba mungu msamaha kabla ya kifo chako

UKIOTA UMEKUFA NA WATU WAMEKUZIKA 

Ishara ya kuishi muda mfupi na utakufa bila kufanya toba. Ila ukiota umekufa ghafla bila kuumwa na hakuna tukio la mazishi utaishi umri mrefu.

UKIOTA UMEKUFA,WATU WANAOMBELEZA NA KUKUFANYIA SHUGHLI ZA MAZISHI

Dunia yako itakuwa nzuri lakini akhera yako imeharibika.

KUOTA MAITI INAJIOSHA YENYEWE

Watu wako watatoka kwenye majonzi na mali yao itazidi. Kama kuna mgonjwa atapona kama mnadaiwa mtalipa kama mwadaiwa mtalipa.

 UKIOTA MAITI IMEVISHWA SANDA  ILA HAIJAKAMILIKA UVAAJI WAKE

Utatiwa kwenye majaribu mazito ya zinaa na mtu wako wa karibu  lakini hutokubali. Ukiota umeona sanda pekee ni ishara ya zinaa inakuja mbele yako ukimuota mkeo mumeo anavishwa sanda na haijakamilika jua ana mipango ya kuzini au ana zini.

UKIOTA UMEFUNGWA KWENYE SANDA VILEVILE KAMA MAITI

Ni ishara ya kifo chako hivyo jibiidishe kufanya ibada kuwaomba radhi uliowakosea 

KUOTA UPO KWENYE JENEZA

Utajenga udugu na mtu kwa ajili ya mungu hivyo kuwa makini na aina ya marafiki ulonao

UKIOTA UPO KWENYE JENEZA NA WATU WAMELIBEBA IMA UMEKUFA AU HUJAFA

Utatawala na kupanda daraja na watu watakufuata kama ulivyowaona ndotoni na pia ni ishara ya kuwashinda maadui zako

UKIOTA UMEBEBA MAITI NA UNAPITA NAE KATIKA NJIA ZISIZO SAHIHI

Utapata mali ya haramu na hutajali upatikanaji wake

UKIOTA UNAMPELEKA MAITI SOKONI

Utapata mahitaji yako na faida kwenye biashara zako

UKIOTA JENEZA LINAPITA HEWANI

Atakufa mtu mkubwa kama rais,mwanachuoni au yeyote mwenye daraja ya juu katika jamii yako

UKIOTA UMEKUFA NA UNAZIKWA 

Utasafiri safari ya mbali na utapata mali

Ukiota umekufa na ukafufuka au kuwa hai ni ishara ya kuwa utaondokana na ufukara au kurejea mtu aliyekwenda mbali 

KUOTA UMEMFUFUA MAITI

Utamsilimisha mtu wa dini nyingine kuwa muislam au mtu muovu atatubia dhambi zake kwako

Kwa wenye maswali uliza hapo chini usinifuata inbox

Kama umelielewa somo na kulipenda andika asante ili tujue tuna umuhimu wa kuandaa chapisho lingine pia waweza shea na wenzio

Kwa wenye matatizo maalumu ya afya. Nyota kazi mapenzi kuibiwa nguvu za kiume uzazi nk niachie ujumbe inbox kwa wanaohitaji msaada wa dawa na tiba +255621442936

maelezo soma makala zilizopita

Maswali kuhusu ndoto uliza hapa chini imbox kwa wenye matatizo tu kutafsr ndoto inbox utalpia

Whatsp group n la malpo kwa wanaohtaj

Comments

  1. Ukiota umekufa na maiti yako inaoshwa na mkeo akiwa na mwanao ila hakuna dalili ya majonzi wala hakuna tukio la kuzikwa inamaana gani

    ReplyDelete
  2. Mke wangu kaota kamuona maiti katika chumba flan nayule maiti akageuka kumtizama.mke wangu alipokimbia nje akamkuta yule maiti anatembea.

    ReplyDelete
  3. Km umefiwa na mumeo afu ukaota kakutokea anakukataza kwa msisitizo kitu flan inakuaje??

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI