NAMNA YA KUJITWAYARISHA KUKOGA JANABA HDHI NA NIFASI
BAADA ya kuongelea madhara yampatayo mtu kwa kutokuoga nifasi hedhi na janaba sasa tufahamu jinsi ya kujitwayarisha hayo majosho au kuoga.
Ufuate mashart ya udhu yaani maji ya kufanyia shughuli hyo yawe twahara, maji hayo yawe halisi yasiwe maji ya kutengeneza, maji hayo yawe yako yasiwe ya kuiba wala kupora kwa mtu, uondoe vtu ambavyo viatafanya maji yasiingie mwilini kama nywele za bandia kucha za bandia mafuta mazito ya ngozi na utoe nguo ngumu yaan ubaki mtupu.
JINSI YA KUOGA JANABA
Unaanza kwa kutia Niyyah nia si lazima utamke kwa saut yatakiwa moyon ville unapotoka tu ndani kwenda choon na ukasema naenda kujitwayarisha na janaba tayar yatosha kuwa nia au kwa kuongezea utasema nanuia kujiywayarisha na jana kiarabu husemwa nawaitu twaharatul janaba utatia kimoyomoyo.
Kisha utaanza kunawa mikono yako kabla ya kuitumbukiza katika chombo,halafu unaosha sehemu zako za siri Hakikisha umenawa vzur tupu yako zile athari za jimai ziwe zimetoka bimaana mbegu za kiume 'shahawa'
Kisha unatawadha udhuu kaamil kama mtu ambaye aenda kuswali ila hapa bismillah utaitamka moyoni pasi kukisirisha kwa saut kwa sababu upo choon hairuhusiki kupiga bismillah kwa saut chooni.
Ukimaliza kutia udhuu unajimwagia maji kichwani mara tatu na uingize au upitishe vidole vyako katika nywele hadi uhakikishe maji yamefika katika ugozi wa kichwa
Mwisho unakamilisha kwa kujimwagia maji kiwiliwili chote huku ukianzia upande wa kulia mara tatu,vile vile upande wa kushoto mara tatu yaani uhakikishe maji yameenea kila sehemu ya kiwiliwili chako imma kwa kujisugua au kutojisugua
Kufikia hapo josho lako limekamilika na unaweza kuswali namna hiyo
NAMNA HII WANAOGA JINSIA YOTE WANAUME NA WANAWAKE.
KUJITWAYARISHA HEDHI NA NIFASI
Hii inawahusu kina mama kama unaavyojua hedhi ni ada ya mwanamke kila mwez lazima atokwe na damu ikiwa wewe hupati hedhi na huna mimba wala hujaweka vizuizi hvyo vya kisasa ambavyo vina madhara ni tatzo pia. Na nifasi ni damu ile inayomtoka mwanamke baada ya kujifungua.
Weng wamezoea kuoga nifasi siku ya 40 baada ya kujifungua lakini kinachotakiwa ni pale tu damu inapokata ujitwayarishe.
Muogaji atakiwa awe pamba au kitambaa cheupe aingize kwenye tupu yake na ahakikishe kabisa hakuna athari za damu ndio aanze zoez la kuoga. Uogaji wake hauna tofaut na janaba ila hapa kichwa chako kiwe na uwezo wa kuongia maji na kikaagusa ngozi ni bzur ukazifumua nywele zako.
Utatia nia kama nilivyoeleza hapo juu na utafuata maelezo yote km ilivyo hapo juu uhakikishe mwili wako umeenea maji mwili mzima.
Kama atakuja mtu kukuosha basi nia uitie mwenyewe asiktilie yule muoshaji
MAMBO YA KUZINGATIA
Vitu vyotr hvyo yaan kujitwayarisha na janaba hedhi na nifasi kuna nguzo kuu ambazo ni mbili ya kwwnza ni kutia nia na ya pili uhakikishe mwili mzima umeenea maji kila upenyo
mwanamke akioga janaba kama amesuka nywele za kawaida tu yaswihi lakini akiwa na hedhi au nifas yampasa afumue nywele zake.
Kwenye kutua udhu ukimaliza ile dua baada ya udhu usiisome mule choon utaisoma baada ya kutoka na ile bismillah usiitoe kwa saut wakat waanza udhu. Au kwa wepes ukimaliza kuosha tupu yako toka nje ya choo tia udhu wako kamili bimaana kisirisha bismillah kwa saut kisha lete dua baada ya udhu kisha ingia choon malizia sehem iliyosalia.
Kwa kuwa umetia udhu kamili kama unaelekea kuswali baada ya kuoga hayo majosho unaruhusiwa kuswali usitie tena udhu labda uwe umeutengua njiani
+255621442936
Comments
Post a Comment