MBWA KATIKA ULIMWENGU WA NDOTO NINI TAFSIRI NA MAANA ZAKE



SABARKHAYR mpendwa mfuatiliaji wa darasa zangu za ndoto tiba nyota na mambo mengine muhimu kwa mwanaadamu leo nakuletea tafsiri ya ndoto za kuwaona mbwa anayekuletea masomo haya ni Mtabibu ASILI TZ.


Ukimuona au kuwaona mbwa wanapigwa na mtu ni ishara ya kuwa siku zijazo utakuwa na ugomvi na mtu wako wa karibu kadri idadi ya mbwa watakavyokuwa wengi ndivyo ukubwa wa ugomvi utakavyokuwa. Ukiwaona mbwa wenyewe wanashambuliana ni ishara ya maadui zako au jamaa zako wenye ubaya na wewe kugombana wenyewe.

Ukiona mbwa amekufa au wamekufa ni ishara ya  mabalaa ugonjwa kwa watu wako karibu kufa msingi kutatokea ugomvi wa ndugu jamaa au wafanyakazi wenzio, ukiwaota watu wanaua mbwa au mbwa mgonjwa ndoton kama n mfanyabiahsra kuna hasara pia ishara nyengine mtoto ataumwa ugomvi katika ndoa kununiwa na wazazi na jamaa wa karibu.

 Kama mbwa anabweka ktk ndoto, inamaanisha kwamba muotaji ni fidhuli na mwenye tabia ya karaha na kuchukiza. Kuumwa na mbwa au kuparurwa inamaanisha madhara yatayosababishwa na adui yako Na ukubwa wa uadui wake unaendana na maumivu uliiyoyahisi kutokana na mtafuno ule. Pia kuumwa na mbwa kuna ishara ya kusumbuliwa na maumivu ya kichwa ambayo yatachosha mwili na hii sihiri itajayotoka kwa adui zako. Idadi na ukubwa wa jeraha ndio idadi ya maadui zako na ukubwa wa tatzo litakalotokea.

Ikiwa utashambuliwa na mbwa lakini hata kudhuru hujapata jeraha hajakuuma wala kukwarua tarajia wageni ambao hujawaona kwa muda mrefu. Washiriki wenzio jambo fulan siku za nyuma, au wanafunzi wa darasa, marafiki wa zamani au wafanya kazi pamoja.

Ukiota unakimbizwa na mbwa ni ishara ya uadui unaokutafuta ikiwa mbwa amefanikiwa kukuzuru uadui uliofanikiwa na maadui zako wana nguvu ikiwa umemshinda ni ishara ya ushnd kwa maadui zako. Pia kukimbizwa na mbwa ugomvi kupigana na mtu uliyempenda pia kama ahad haitatimia na mtu hatarejea.

Ukiota mbwa anachana nguo ya mtu au yako inamaanisha kwamba mtu muovu anamsengenya ama adui yako yupo katika mazungumzo ya kuaandaa njama za kukidhuru. Ukiota mbwa anakuletea fujo anakukera ni ishara ya migogoro itakayokukosesha raha.

Ukiota mbwa anazungumza ni ishara kuongopewa na watu wa karibu ishara ya kutapeliwa kama una mipango na makampuni ya nje haitakaa sawa na utapigwa pesa pia kuna uadui wa kutegeshewa wakat wa jion ikiwa ni mtu wa kirud nyumban usiku usipende kupita njia moja kila siku pia penda kutulia nyumban nyakat za usiku mpaka utakapopata ufumbuzi.

Katika ndoto mbwa pia anamaanisha ukafiri, kukata tamaa, khofu, jela au kutoroka. Kumuona mbwa ktk mji katika ndoto vile vile inamaanisha kufunga mkataba mpya wa biashara. Ukimuona mbwa mkubwa sana utapata rafiki mpya muamnifu na atakusaidia mambo yako, ikiwa wamuona mbwa mdogo ndotoni kinyume chake.

Ikiwa unamuona mbwa anavyokua yaan umemuona mbwa mdogo mpaka anakua katika ndoto ni ishara ya kuzungumzwa kwa wema na marafiki zako na wanaongea kipindi ambacho haupo.

Ukimuona mbwa na paka wamekaa sehem moja ni ishara ya maadui zako wameungana na wanaoanga njama za kukudhuru pia kama umegombana na mkeo au mumeo ni ishara mbaya hiyo.

Mambo muhimu angalia matendo makuu ndani ya ndoto yako angalia ishara unazoota ndotoni ndizo zinazoleta tafsir kamili

Maswali kuhusu ndoto uliza hapa chini inbox utagharamia 

Una tatzo lolote la afya uzazi nguvu za kiume kesi kuibiwa bishara nk niachie ujumbe inbox

+255621442936 
Group la whatsp ni la malpo 

Comments

  1. Nimeota mbwa watatu wanabweka lakini hawajanidhuru ila wamemdhuru rafiki yangu mbwa niwa kubwa kabisa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jitahd kusoma vzur maelezo yote uliyoayuliza yamefafanuliwa hapo juu

      Delete
  2. Nimeota nimesimama katika nyumba yetu ya familia na nimenyoosha mkono kuelekea dirishani na kusoma Suratul Ihlas mara 3, kisha nikajikuta ninatembea katika maeneo ninayo yafahamu huku mbwa mwekundu,mkubwa na mzuri sana ananifuata kwa nyuma na nikimwambia arudi alikotoka anafanya kugeuka kama anataka kurejea alikotoka ila kisha anasita na kuendelea kunifuata baada ya mimi pia kuanza kwenda zangu na safari zangu

    ReplyDelete
  3. Mimi nimeota nipo na mwanaume ninayeishi nae ndani alikuwa kaziba mlango wa kutokea na kitu apo chini mimi kikaenda kukitoa wakaja mbwa mweusi mmoja wa rangi nyingine moja na mtoto wa mbwa mmoja wanabweka sana hawa wakubwa nawapiga sana ila hawaingii ndani wanabweka tuu

    ReplyDelete
  4. Mwanangu wa miaka 6 ameota amepalulwa na mbwa alafu mbele yake kuna watu wawili wamesimama wanamuangalia na mbwa hajawazuru

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI