NDOTO ZA VIFO NA KUWAOTA WATU WALIOKUFA


HABARI yako mpenzi mfuatiliaji wa darasa zetu kupitia ukurasa wetu huu wa mtabibu asili tz. Tunapenda kuwajulisha kuwa kila swali liulizwe chini ya mada husika usilete maswali inbox. Inbox kwa wati wenye shida maalumu tu za kufanya kazi pili kila kitu tunachokizungumza tunaweka na ushauri au jinsi ya kumaliza tatizo chini ya mada husika ikitokea unahitaji msaada wa kiofisi si bure hii ni kazi heshima iwepo.


Twende kwenye tafsiri za ndoto za vifo. Hapa namaanisha muotaji ukiota umekufa au kuota maiti kuota upo mazishini kuota mtu aliyekufa yaani kwa kifupi ni ndoto zote zinazohusisha kifo.

Kifo ni mwisho wa maisha ya mwanadamu ya kidunia mtu akifa anaenda kuanza maisha mapya ambayo ni siri mimi na wewe hatuayajui. Kwa maana hiyo tafsiri ya ndoto za kifo mara nyingi huwa ni mwisho wa jambo fulani yaweza ikawa mwisho wa huzuni ikaja furaha, yaweza ikawa mwisho furaha ikaja huzuni, yaweza ikawa mwisho wa biashara yako mwisho wa ndoa yako mwisho ufukara kwenda utajiri nk.
Hivyo kuwa makini katika tasfiri zifuatazo hapo chini.

UKIOTA WATU WALIOKUFA
Ukiota mtu aliyekufa anaumwa au hali yake mbaya ama anakuomba msaada wa kitu chochote iwe fedha chakula nk ujue huko alipo hali yake si nzuri ana adhabu hivyo mfanyie visomo sana mtoleen sadaka. Ukiota mtu aliyekufa ana furaha sana anakupa wewe msaada wa kitu chochote ujue alipo ana neema endeleeni kumuombea dua.

Ukiota watu/mtu aliyekufa amesimama  bombani au kisimani anakunywa maji ni ishara ya kutokea maradhi mabaya kwa ukoo au jamii ya muotaji bimaana eneo analokaa aliyeota. Ukiota maiti nyingi zinatoka makaburini na kuja kugombea chakula ni ishara ya kupanda bei vitu vya kula.

Ukiota mtu aliyekufa amekufa tena alafu anarudi kuja keluwatembelea ni ishara ya kifo kwa huyo mtu aliyetembelewa hivyo ajibidiishe kwenye heri na toba kwani kifo chake kimekaribia.

Ukiota mtu amekufa wakati kiuhalisia yuhai basi mtu huyo muheshimu ana mchango mkubwa kwenye maisha yako baadae na atakupeleka njia salama ya mungu.

Ukiota mtu aliyekufa anamuombea mtu maiti mwenzie basi wewe muotaji unajipatia fedha zako kwa njia zisizo halali na unapenda uongo rejea kwwnye njia za halali

Ukiota mtu aliyekufa anazama kwenye maji ni ishara ya wewe kujihusisha na vitendo vya dhambi visivyompendeza mungu.

Ukiota watu waliokufa wanauza bidhaa au biashara ni ishara ya kudorora biashara yako au kazi yako au kupata shida kwenye utafutaji wako.
Ukiota umelala kitanda kimoja na mtu aliyekufa ni ishara ya kuishi muda mrefu.

Ukiota unamfuata maiti na mnatembea pamoja kwa kushikana mikono hiyo ni ishara ya kunyooka mipango yako na utapata pesa katika njia ambazo hukuzitegemea.

Ukiota mtu aliyekuwa mashughuli katika ukoo au jamii mnaongea vizuri ukambusu au akakubusu basi ni ishara ya wewe kupata umaarufu na kuishi kama alivyoishi huyo maiti.

Mwanamke ambaye ameolewa akiota maiti kwenye ndoto ni ishara ya ndoa yake kuingia matatizoni na kuvunjika hii pia hata kwa wanaume ndoto hii huambatana na ndoto ya kung'oka jino la chini la mbele ikifikia unaota sana jino linang'oka wewe subiri siku tu na saa ndoa lazima itavunjika.
Na kwa mawanamke ambaye hajaolewa akaiota anaolewa na maiti ni ishara ya kupata ndoa.

Kwa leo tuishie hapa nitaendelea siku zijazo ndoto za wewe mwenyewe kuota umekufa. Unashonewa sanda upo kaburini. Unafufuka ndoto za kuota watu walio hai wamekufa tutazitafsiri pia ila kama umeliewa hili somo andika asante hapo chini ili iwe rahisi kuandaa hayo masomo niliyotaja ukikaa kimya najua hakuna umuhimu wa kuendelea

Maswali kuhusu ndoto nilizofafanua tu yaulizwe hapo chini. Mjitahd kusoma maelezo kuna maswalu mengine mnauliza hakuna tofaut na maelezo niliyoyatoa pia angalia maswali ya mwenzio swali moja sijibu mara mbili

Mfano nimeeleza ukimuota mtu aliyekufa ana hudhun au anaomba kitu chochote au yupo kwenye hali ya uchafu unmesema tafsiri yake mtu huyo yupo katika hali ngumu kaburini mwatakiwa mumfanyie kisomo 
Unakuta mtu anauliza nmemuota baba angu kavaa nguo zimechanika hii inamaana gani 

Jitahdn kusoma msikimbilie kuuliza maswali

 Mwenye shida binafsi aniachie ujumbe inbox
Wabillah tawfiq tuzidishi ibada kila nafsi itaonja umauti

+255621442936

Ukiota umekufa soma maelezo yake hapa http://tabibuasili.blogspot.com/2020/08/ukiota-umekufa-ukiota-unaona-maiti.html

Comments

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI