NDOTO ZA NYUMBA, UKIOTA UNAJENGA UMEBOMOKEWA UNAUZA NK FAHAMU MAANA ZAKE


SABAR KHAYR mpenzi mfuatiliaji wa mfululizo wa darassa zangu zinazohusiana na dawa asili ndoto na maradhi kwa ujumla. Leo tutazungumzia kuhusiana na ndoto zinazohusu nyumba. Yaan umelala ukaota ndoto inayowasilisha nyumba ndani yake.


Ndoto hizi ninazotafsir zinawahusu binaaadamu wote isipokuwa yule fundi wa ujenzi wa nyumba ikiwa shughuli zako ni ujenzi wa nyumba. Ubongo wako utakuwa umekariri kazi zako kwako wewe kuota unajenga ni jambo la kawaida ila ikitokea ukawa unaota mara kwa mara ndoto zinazohusiana na nyumba na wewe ni fundi ujenzi yakupasa usome kwa makini maneno hayo chini.

Ukiota unajenga nyumba ni ishara ya mafanikio katika kazi biashara utapata mafanikio milango ya ndoa ipo waz utaoa na utapata furaha. Ukiota unabomowa nyumba ni ishara ya mitihan mambo yako hayatakaa sawa. Ukiota unabomokewa na nyumba yaani nyumba imebomoka upo ndani na watu wanakuona ni ishara ya kutoka siri zako kama una ahad pahala basi haitatimia au kupata nusu hata ukimuotea mtu kabomokewa na nyumba ni hvyo.

Ukiota nyumba yako imeteketezwa aidha kwa moto au chochote utasumbuliwa na wenye mamlaka lakini pia ni ishara ya maradhi ya mripuko. Ukiota unauza nyumba ni ishara ya ukomo wa jambo fulan yaweza ikawa ni maisha yako au shughuli unayoifanya. Ukiota umenunua nyumba ni ishara ya kutimia mipango yako kama kuna kes utashinda bila pingamizi.


Ukiota umehamia kwenye nyumba mpya lakini hyo nyumba haina madirisha wala milango mingi mlango ni wakuingia tu ni tafsri upo katika hali mbaya tena yaweza kuwa umaut upo karibu jibiidishe na ibada za kufanya toba. Ukiota unapamba nyumba ni faidia kuna familia inaongezeka utapata watoto.

Ukiota unaona nyumba iliyojengwa kwa mbao ni ishara ya ustawi afya njema kwa muotaji nahusiano mazuri kwa ndugu na jamaa zake, ukiota waona nyumba kubwa ya tofali ina vyumba vingi ni ishara ya kinga kuwa imara dhidi ya maadui zako. Ukiota upo nyumbani kwa baba au mama na ulihama zamani inaashiria mambo mawili jambo la kwanza ni masuala ya urithi au taarifa kutoka upande ulioota, unaweza pata taarifa ya her au shaari. Ukiota upo katika nyumba ya baba au mama na umerud utotoni ni ishara ya vifungo husda na matambiko hapa yategemea na maangalizi zaidi na upande uliouta ndio wenye tatizo lako ikiwa mambo yako hayaend basi rud haraka.

Ukiota kiumbe cha ajabu au jini limesimama pembezon mwa nyumba yako ni ishara ya muotaji kuwa dhalili, unyonge, kupata hasara na hapa kuna ahadi au nadhiri uliiweka hukitimiza. Ukiota wachawi au majini yamevamia nyumbani kwako na kufanya uharibifu ni ishara ya wez au maadui wataingia ndani kwako aidha kuiba au kutimiza kile walichokusudia. Hapa hata ukiota nyumba ya mtu awe jamaa au ndugu yako tafsiri yake ni hyohyo huyo uloyemuota ndiye atakayekumbwa na mitihan hyo.


Ukiota umesimama juu ya ukuta ni ishara ya uongozi au kuwa juu kimaarifa iwapo muotaji ataota kwenye ukuta ulioporomoka atakuwa ni kiongozi wa udhalimu na uhatibif wa mali za watu.


Ukiota mlango una anguka au kufunguka wenyewe ni ishara ya muotaji kuoata mitihani ya maradhi ila utapona. Ukiota una ufunga mlango wa nyumba yako au ulipopanga kama n mume utamtaliki mkeo na kama ni mke basi ataidai talaka mwenyewe.

Tutoe nyongeza ya mchanga vumbi na kokoto. Ukiota unatembea juu ya mchanga au kushika kuokota mchanga muotaji atapa mali lakini yampasa afanye kazi ngumu sana za sulubu. Mchanga au vumbi kupeperuka hewani ni ishara ya mipango kutotimia ukiota mchanga vumbi au udongo unakufuata na kukumba ni neema utaipata katika mambo yako.

  MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
ukiota hakikisha unafuatilia ndoto zako hasa zile zinazojirudia. Ukiota ndoto za mbaya usimuhadithie mtu hima yule mtafsiri tu. Na ndoto ambazo zina matendo mengi ndani yake mpaka hukumbuki mwanzo wala kati ni ndoto za kichawi tu. Mtu ambaye hakumbuki ndoto zake au haoti kabisa ni ishara moja wapo ya kifungo.

Wale watu wa Dar es salaam wenye matatizo yao mwnzon mwa mwez ujao bimaana mwez wa tisa nitakuwa hapo eleza shida yako mapema na weka ahad ili nikija nijue nabeba nini na nn

Maswali kuhusi ndoto yaulizwe hapa chini inbox utalipia

Una tatzo lolote la uzazi guvu za kiume biashara mapenzi kesi kuuza kuibiwa nk niachie ujumbe inbox

+255621442936 kwa mesej za whatsp ama kupga

Whatsp group ni la malipo kwa wahtaj

Comments

  1. Nimeota kati ya nyumba zangu tatu zilizo ambatana mbili zimebomoka imebaki ya katikati na moja imebomoka umebaki ukutakidogo sasa na watu natafakari muongeze tofauti upande lakini umelowa sana .

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAFUSHO MADINI YA KILA NYOTA NA JINSI YANAVYOTUMIKA

NDOTO ZA FEDHA NA TAFSIRI ZAKE UKIOTA UMEOKOTA HELA. UKIOTA UMEDONDOSHA HELA. UKIOTA UNAPEWA HELA

FAHAMU KUHUSU MTI NDULELE TURA FAIDA NA MATUMIZI KATIKA AFYA NA MAPENZI